Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Samsoni
Waamuzi 16 : 31
31 Ndipo ndugu zake, na watu wote wa nyumba ya baba yake wakateremka, wakamtwaa wakamchukua, wakamzika kati ya Sora na Eshtaoli, katika kiwanja cha kuzikia cha Manoa baba yake. Naye alikuwa mwamuzi wa Israeli muda wa miaka ishirini.
Waamuzi 13 : 7
7 lakini aliniambia, Tazama, utachukua mimba, nawe utamzaa mtoto wa kiume; basi sasa, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi. Maana mtoto huyo atakuwa Mnadhiri wa Mungu tangu tumboni, hadi siku ya kufa kwake.
Waamuzi 13 : 25
25 Roho ya BWANA ikaanza kumtaharakisha katika Mahane-dani, katikati ya Sora na Eshtaoli.
Waamuzi 14 : 7
7 Basi akateremka na kuzungumza na huyo mwanamke; naye akampendeza Samsoni sana.
Waamuzi 14 : 19
19 Roho ya BWANA ikamjia juu yake kwa nguvu, naye akateremka hadi Ashkeloni, akawaua wanaume thelathini katika watu hao, na kuzitwaa nyara zao, na kuwapa hao waliokitambua kitendawili mavazi hayo ya sikukuu. Hasira zake zikampanda, naye akakwea kwenda nyumbani kwa baba yake.
Waamuzi 14 : 19
19 Roho ya BWANA ikamjia juu yake kwa nguvu, naye akateremka hadi Ashkeloni, akawaua wanaume thelathini katika watu hao, na kuzitwaa nyara zao, na kuwapa hao waliokitambua kitendawili mavazi hayo ya sikukuu. Hasira zake zikampanda, naye akakwea kwenda nyumbani kwa baba yake.
Waamuzi 14 : 20
20 Lakini huyo mke wa Samsoni aliozwa mwenzake, ambaye alikuwa amemtendea kama rafikiye.
Waamuzi 15 : 2
2 Baba yake akasema, Hakika mimi nilidhani ya kuwa umemchukia kabisa; basi nilimpa rafiki yako. Je! Si dada yake mdogo ni mzuri kuliko yeye? Tafadhali, mtwae huyo badala yake.
Waamuzi 15 : 8
8 ② Ndipo akawashambulia vikali na kuwaua wengi, kisha akateremka na kukaa katika ufa wa jabali la Etamu.
Waamuzi 15 : 14
14 Alipofika Lehi, Wafilisti wakapiga kelele walipokutana naye; ndipo Roho ya BWANA ikamjia kwa nguvu, na zile kamba zilizokuwa juu ya mikono yake zikawa kama kitani iliyoteketezwa kwa moto, na vile vifungo vyake vikaanguka mikononi mwake.
Waraka kwa Waebrania 11 : 32
32 ⑥ Nami niseme nini tena? Maana wakati usingenitosha kuleta habari za Gideoni na Baraka na Samsoni na Yeftha na Daudi na Samweli na za manabii;
Waamuzi 15 : 17
17 Ikawa, alipokuwa amekwisha kunena akautupa ule mfupa wa taya mkononi mwake; na mahali pale pakaitwa Ramath-lehi.[13]
Leave a Reply