Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia sala ya kimya
Mathayo 6 : 6
6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
1 Samweli 1 : 12 โ 13
12 Ikawa, hapo alipoendelea kuomba mbele za BWANA, Eli akamwangalia kinywa chake.
13 Basi Hana alikuwa akinena moyoni mwake; midomo yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe; kwa hiyo huyo Eli alimdhania kuwa amelewa.
Mwanzo 24 : 45
45 Hata kabla sijaisha kusema moyoni mwangu, tazama! Rebeka akatokea, na mtungi begani mwake. Akashuka kisimani akateka. Nami nikamwambia, Tafadhali nipe maji ninywe.
Leave a Reply