Biblia inasema nini kuhusu Sadaka ya Kila Siku – Mistari yote ya Biblia kuhusu Sadaka ya Kila Siku

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Sadaka ya Kila Siku

Kutoka 29 : 42
42 Itakuwa ni sadaka ya kuteketezwa milele katika vizazi vyenu vyote mlangoni pa ile hema ya kukutania mbele ya BWANA; hapo nitakapokutana nanyi, ili ninene na wewe hapo.

Kutoka 30 : 9
9 Hamtafukiza juu yake uvumba mgeni, wala sadaka ya kuteketezwa, wala sadaka ya unga, wala hamtamimina juu yake sadaka ya kinywaji.

Hesabu 28 : 8
8 Na mwana-kondoo wa pili utamsongeza wakati wa jioni; kama ile sadaka ya unga iliyosongezwa asubuhi, na kama sadaka yake ya kinywaji, ndivyo utakavyoisongeza, ni sadaka ya kusongezwa kwa moto, ni harufu ya kupendeza kwa BWANA.

Ezra 3 : 6
6 Tangu siku ya kwanza ya mwezi wa saba walianza kumtolea BWANA sadaka za kuteketezwa, lakini msingi wa hekalu la BWANA ulikuwa haujawekwa bado.

Ezekieli 46 : 15
15 Hivyo ndivyo watakavyomtoa mwana-kondoo, na sadaka ya unga, na mafuta, kila siku asubuhi, kuwa sadaka ya kuteketezwa ya daima.

Danieli 9 : 21
21 naam, nilipokuwa nikinena katika kuomba, mtu yule, Gabrieli, niliyemwona katika njozi hapo kwanza, akirushwa upesi, alinigusa panapo wakati wa dhabihu ya jioni.

Danieli 9 : 27
27 ① Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.

Danieli 11 : 31
31 Na wenye silaha watasimama upande wake, nao watapatia unajisi mahali patakatifu, ndiyo ngome, nao wataondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, nao watalisimamisha chukizo la uharibifu.

Yohana 1 : 29
29 Kesho yake alimwona Yesu akija kwake, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu, aichukuaye dhambi ya ulimwengu!

Yohana 1 : 36
36 ④ Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu!

1 Petro 1 : 19
19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na dosari wala waa, yaani, ya Kristo.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *