Biblia inasema nini kuhusu sabato – Mistari yote ya Biblia kuhusu sabato

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia sabato

Kutoka 31 : 13 – 17
13 ④ Kisha, nena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati yenu na mimi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi.
14 ⑤ Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hana budi atauawa; na kila mtu afanyaye kazi siku hiyo, ataondolewa toka kwa watu wake.
15 ⑥ Kazi itafanywa siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, takatifu kwa BWANA; kila mtu atakayefanya kazi yoyote katika siku ya Sabato, hana budi atauawa.
16 Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika Sabato, kuiangalia sana hiyo Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele.
17 ⑦ Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita BWANA alifanya mbingu na nchi, akapumzika kwa siku ya saba na kustarehe.

Kutoka 20 : 8 – 11
8 ⑳ Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;
10 lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako.
11 Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.

Marko 2 : 27
27 ⑪ Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato.

Kutoka 31 : 13
13 ④ Kisha, nena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati yenu na mimi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi BWANA niwatakasaye ninyi.

Luka 23 : 56
56 ⑭ Wakarudi, wakatayarisha manukato na marhamu. Na siku ya sabato walistarehe kama ilivyoamriwa.

Mwanzo 2 : 3
3 Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.

Luka 4 : 16
16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.

Matendo 17 : 2
2 Na Paulo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimokuwa, akahojiana nao kwa maneno ya Maandiko sabato tatu,

Waraka kwa Waebrania 4 : 9
9 Basi, limesalia pumziko la sabato kwa watu wa Mungu.

Luka 6 : 1 – 20
1 ⑬ Ikawa siku ya sabato moja alikuwa akipita katika mashamba, wanafunzi wake wakawa wakivunja masuke na kuyala, wakiyapukusapukusa mikononi mwao.⑭
2 ⑮ Basi baadhi ya Mafarisayo wakawaambia, Mbona mnafanya lisilo halali siku ya sabato?
3 ⑯ Yesu akawajibu akawaambia, Hamkulisoma hata hilo alilolifanya Daudi, alipokuwa na njaa, yeye na wale aliokuwa nao?
4 ⑰ Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaitwaa mikate ile ya wonyesho, akaila akawapa na hao wenziwe, ambayo si halali kuila ila kwa makuhani peke yao.
5 Akawaambia, Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato.
6 ⑱ Ikawa siku ya sabato nyingine aliingia katika sinagogi akafundisha; na mlikuwamo mtu ambaye mkono wake wa kulia umepooza.
7 ⑲ Na Waandishi na Mafarisayo walikuwa wakimvizia, ili waone kama ataponya siku ya sabato; kusudi wapate neno la kumshitakia.
8 Lakini yeye akayatambua mawazo yao, akamwambia yule mwenye mkono uliopooza, Ondoka, simama katikati; akaondoka akasimama.
9 Ndipo Yesu akawaambia, Nawauliza ninyi, Je! Ni halali siku ya sabato kutenda mema, au kutenda mabaya; kuponya roho au kuangamiza?
10 Akawakazia macho wote pande zote, akamwambia yule mtu, Nyosha mkono wako. Akaunyosha; mkono wake ukawa mzima tena.
11 Wakajawa na uchungu, wakashauriana wao kwa wao wamtendeje Yesu.
12 ⑳ Ikawa siku zile aliondoka akaenda mlimani ili kuomba, akakesha usiku kucha akimwomba Mungu.
13 Na kulipokucha aliwaita wanafunzi wake; akachagua kumi na wawili miongoni mwao, ambao aliwaita mitume;
14 Simoni, aliyemwita jina la pili Petro, na Andrea nduguye, na Yakobo na Yohana, na Filipo na Bartholomayo,
15 na Mathayo na Tomaso, na Yakobo wa Alfayo, na Simoni aitwaye Zelote,
16 na Yuda wa Yakobo, na Yuda Iskarioti, ndiye aliyekuwa msaliti.
17 Akashuka pamoja nao, akasimama mahali tambarare, pamoja na wanafunzi wake wengi, na makutano makubwa ya watu waliotoka Yudea wote na Yerusalemu, na pwani ya Tiro na Sidoni; waliokuja kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao;
18 na wale waliosumbuliwa na pepo wachafu; waliponywa.
19 Na makutano yote walikuwa wakitaka kumgusa, kwa sababu uweza ulikuwa ukimtoka ukiwaponya wote.
20 Akainua macho yake akawatazama wanafunzi wake, akasema, Heri ninyi mlio maskini, kwa sababu ufalme wa Mungu ni wenu.

Isaya 58 : 13
13 Kama ukigeuza mguu wako usiivunje sabato, usifanye anasa yako siku ya utakatifu wangu; ukiita sabato siku ya furaha, na siku takatifu ya BWANA yenye heshima; ukiitukuza, kwa kutokuzifanya njia zako mwenyewe, wala kuyatafuta yakupendezayo, wala kusema maneno yako mwenyewe;

Matendo 16 : 13
13 Siku ya sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tulidhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.

Isaya 66 : 23
23 ⑫ Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA.

Marko 2 : 28
28 Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa sabato pia.

Mathayo 24 : 20
20 Ombeni, ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato.

Luka 23 : 54
54 Na siku ile ilikuwa siku ya Maandalio, na sabato ikaanza kuingia.

Matendo 18 : 4
4 Akatoa hoja zake katika sinagogi kila sabato, akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wagiriki.

Mwanzo 2 : 2
2 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya.

Ezekieli 22 : 8
8 Umevidharau vitu vyangu vitakatifu, umezitia unajisi sabato zangu.

Luka 4 : 31
31 Akashuka mpaka Kapernaumu, mji wa Galilaya, akawa akiwafundisha siku ya sabato;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *