Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Saba
Mwanzo 2 : 3
3 Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.
Kutoka 20 : 11
11 Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.
Kumbukumbu la Torati 5 : 14
14 ⑥ lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala ng’ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako yeyote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, ili mtumwa wako na mjakazi wako wapumzike vile vile kama wewe.
Mwanzo 7 : 4
4 ⑩ Kwa maana baada ya siku saba nitainyeshea dunia mvua, siku arubaini mchana na usiku; na kila kilicho hai nilichokifanya juu ya uso wa nchi nitakifutilia mbali.
Mwanzo 7 : 10
10 Ikawa baada ya siku hizo saba, maji ya gharika yakawa juu ya nchi.
Mwanzo 8 : 10
10 Akangoja na siku saba tena; kisha akamtoa yule njiwa katika safina mara ya pili,
Mwanzo 8 : 12
12 Akangoja na siku saba tena, akamtoa yule njiwa; naye asimrudie tena kamwe.
Mwanzo 50 : 10
10 ⑬ Wakaja mpaka uwanja wa kupuria nafaka wa Atadi, uliyo ng’ambo ya Yordani. Wakaomboleza huko maombolezo makuu, mazito sana. Akafanya matanga ya baba yake siku saba.
Ayubu 2 : 13
13 Kisha wakaketi ardhini pamoja naye muda wa siku saba, mchana na usiku, wala hapana mmoja aliyenena naye neno lolote; kwa maana waliona ya kuwa mashaka yake aliyo nayo ni makuu mno.
Kutoka 7 : 25
25 Zikatimia siku saba, baada ya BWANA kuupiga ule mto.
Yoshua 6 : 4
4 Na makuhani saba watachukua baragumu saba za pembe za kondoo dume, watatangulia mbele za hilo sanduku; na siku ya saba mtauzunguka mji mara saba, nao makuhani watapiga baragumu zao.
Kutoka 12 : 15
15 ② Mtakula mikate isiyochachwa muda wa siku saba; siku hiyo ya kwanza mtaondoa chachu yote isiwe katika nyumba zenu kabisa; kwa kuwa mtu yeyote atakayekula mkate uliochachwa tangu siku hiyo ya kwanza hata siku ya saba, nafsi hiyo atakatiliwa mbali na Israeli.
1 Samweli 10 : 8
8 ⑪ Nawe utateremka mbele yangu mpaka Gilgali; nami, angalia, nitakuteremkia huko, ili kutoa sadaka za kuteketezwa, na kuchinja sadaka za amani; siku saba utangoja, hata nitakapokujia, na kukuonesha yatakayokupasa kuyafanya.
1 Samweli 13 : 8
8 ⑬ Akangoja siku saba, kwa kadiri ya muda uliowekwa na Samweli lakini Samweli hakuja Gilgali; na hao watu wakatawanyika mbali naye.
Leave a Reply