Biblia inasema nini kuhusu rushwa – Mistari yote ya Biblia kuhusu rushwa

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia rushwa

Kutoka 23 : 8
8 Nawe usipokee rushwa; kwani hiyo rushwa huwapofusha macho hao waonao, na kuyapotoa maneno ya wenye haki.

Mithali 15 : 27
27 ④ Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe; Bali achukiaye zawadi ataishi.

Mithali 17 : 23
23 Asiye haki hutoa rushwa kifuani, Ili kuzipotosha njia za hukumu.

Mithali 17 : 8
8 Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; Kila kigeukapo hufanikiwa.

1 Timotheo 6 : 10
10 Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.

Amosi 5 : 12
12 ⑰ Maana mimi najua jinsi maasi yenu yalivyo mengi, na jinsi dhambi zenu zilivyo kubwa; ninyi mnaowaonea wenye haki, mnaopokea rushwa, na kuwageuza wahitaji langoni wasipate haki yao.

Mhubiri 7 : 7
7 Kweli jeuri humpumbaza mwenye hekima, Na rushwa huuharibu ufahamu.

Mithali 21 : 14
14 Kipawa cha siri hutuliza hasira; Na rushwa bindoni humliza ghadhabu kali.

Isaya 5 : 23
23 wampao haki mwenye uovu, ili wapewe ijara, na kumwondolea mwenye haki haki yake!

Zaburi 26 : 10
10 Mikononi mwao mna madhara, Na mkono wao wa kulia umejaa rushwa.

Mathayo 28 : 12 – 15
12 Wakakusanyika pamoja na wazee, wakafanya shauri, wakawapa askari fedha nyingi,
13 wakisema, Semeni, ya kwamba wanafunzi wake walikuja usiku, wakamwiba, sisi tulipokuwa tumelala.
14 Na jambo hili likisikika kwa mtawala, sisi tutasema naye, nanyi hamtapata shida.
15 Basi wakazitwaa zile fedha, wakafanya kama walivyofundishwa. Na neno hilo likaenea kati ya Wayahudi hata leo.

Isaya 1 : 23
23 Wakuu wako ni waasi, na rafiki za wezi; kila mtu hupenda rushwa, hufuata malipo; hawampatii yatima haki yake, wala maneno ya mjane hayawafikii.

Ayubu 15 : 34
34 Kwa kuwa jamii ya hao wasiomcha Mungu watakuwa tasa, Na moto utateketeza mahema yenye rushwa.

Mithali 11 : 1
1 Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa BWANA; Bali vipimo vilivyo sawasawa humpendeza.

Mithali 10 : 2
2 ⑦ Hazina za uovu hazifaidii kitu; Bali haki huokoa na mauti.

Mithali 29 : 4
4 Mfalme huithibitisha nchi kwa hukumu; Bali yeye apokeaye rushwa huipindua.

Waamuzi 16 : 5
5 ⑩ Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja.

Mithali 28 : 21
21 ④ Kupendelea watu si kwema; Wala mtu kuasi kwa ajili ya kipande cha mkate.

Yakobo 2 : 7
7 Hawalitukani jina lile zuri mliloitwa?

Kumbukumbu la Torati 16 : 19
19 Usipotoe maamuzi; wala usipendelee uso wa mtu; wala usitwae rushwa; kwa kuwa rushwa hupofusha macho ya wenye akili, na kugeuza kesi wa wenye haki.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *