Biblia inasema nini kuhusu Ribla – Mistari yote ya Biblia kuhusu Ribla

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ribla

Hesabu 34 : 11
11 ⑳ kisha mpaka utateremka kutoka Shefamu mpaka Ribla, upande wa mashariki wa Aini; kisha mpaka utateremka na kufikia upande wa bahari ya Kinerethi[47] upande wa mashariki;

2 Wafalme 23 : 33
33 Naye Farao Neko akamfunga huko Ribla, katika nchi ya Hamathi, ili asitawale huko Yerusalemu. Akaitoza nchi kodi talanta mia moja za fedha na talanta ya dhahabu.

2 Wafalme 25 : 6
6 ⑦ Ndipo wakamkamata mfalme, wakamchukua kwa mfalme wa Babeli huko Ribla; wakatoa hukumu juu yake.

2 Wafalme 25 : 21
21 ⑳ Naye mfalme wa Babeli akawapiga, na kuwaua huko Ribla katika nchi ya Hamathi. Hivyo Yuda wakachukuliwa utumwani kutoka nchi yao.

Yeremia 39 : 6
6 Ndipo mfalme wa Babeli akawaua wana wa Sedekia huko Ribla mbele ya macho yake; pia mfalme wa Babeli akawaua wakuu wote wa Yuda.

Yeremia 52 : 9
9 ④ Nao wakamshika mfalme, wakamchukua kwa mfalme wa Babeli, aliyekuwa huko Ribla katika nchi ya Hamathi, naye akatoa hukumu juu yake.

Yeremia 52 : 26
26 Na Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, akawatwaa, akawaleta kwa mfalme wa Babeli huko Ribla.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *