Biblia inasema nini kuhusu riba – Mistari yote ya Biblia kuhusu riba

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia riba

Kutoka 22 : 25
25 Ukimkopesha mtu aliye maskini, katika watu wangu walio pamoja nawe; usiwe kwake mfano wa mwenye kumdai; wala hutamwandikia faida.

Kumbukumbu la Torati 23 : 19
19 Usimkopeshe ndugu yako kwa riba; riba ya fedha, riba ya vyakula, riba ya kitu chochote kikopeshwacho kwa riba;

Kumbukumbu la Torati 23 : 19 – 20
19 Usimkopeshe ndugu yako kwa riba; riba ya fedha, riba ya vyakula, riba ya kitu chochote kikopeshwacho kwa riba;
20 mgeni waweza kumkopesha kwa riba, ila usimkopeshe ndugu yako kwa riba; ili BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika yote utiayo mkono wako, katika nchi uingiayo kuimiliki.

Ezekieli 18 : 8
8 ambaye hakumkopesha mtu ili apate faida, wala hakupokea ziada ya namna yoyote; naye ameuepusha mkono wake na uovu, na kufanya hukumu ya haki kati ya mtu na mwenzake;

Mambo ya Walawi 25 : 37
37 Usimpe fedha yako upate riba, wala usimpe vyakula vyako kwa kujitakia faida.

Ezekieli 18 : 13
13 ④ naye amekopesha watu ili apate faida, na kupokea ziada; je! Ataishi baada ya hayo? La, hataishi; amefanya machukizo hayo yote; hakika atakufa; damu yake itakuwa juu yake.

Mambo ya Walawi 25 : 35 – 37
35 ⑳ Na ikiwa ndugu yako amekuwa maskini, na mkono wake umelegea kwako, ndipo utamsaidia, atakaa nawe kama mgeni, na msafiri.
36 Usitake riba kwake wala faida, bali mche Mungu wako, ili ndugu yako akae nawe.
37 Usimpe fedha yako upate riba, wala usimpe vyakula vyako kwa kujitakia faida.

Luka 6 : 35
35 Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye Juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.

Ezekieli 18 : 17
17 ⑥ tena ikiwa ameuzuia mkono wake asimwonee maskini, wala hakupokea faida na ziada, naye amezifanya hukumu zangu, na kuzifuata sheria zangu; hatakufa huyu kwa sababu ya uovu wa baba yake, hakika ataishi.

Ezekieli 22 : 12
12 ② Ndani yako wamepokea rushwa ili kumwaga damu; umepokea riba na faida; nawe kwa choyo umepata mapato kwa kuwadhulumu jirani zako, nawe umenisahau mimi, asema Bwana MUNGU.

Mithali 22 : 7
7 Tajiri humtawala maskini, Naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye.

Zaburi 15 : 5
5 Asiyetoa fedha yake apate kula riba, Asiyepokea rushwa amwangamize asiye na hatia. Mtu atendaye mambo hayo Hataondoshwa milele.

Mathayo 25 : 27
27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.

Mambo ya Walawi 25 : 36
36 Usitake riba kwake wala faida, bali mche Mungu wako, ili ndugu yako akae nawe.

Nehemia 5 : 1 – 13
1 Ndipo kukatokea kilio kikuu cha watu, na wake zao, juu ya ndugu zao Wayahudi.
2 Maana, walikuwako watu waliosema, Sisi, na wana wetu na binti zetu, tu wengi; na tupate ngano, tule, tukaishi.
3 Tena walikuwako wengine waliosema, Tumeweka rehani mashamba yetu, na mizabibu yetu, na nyumba zetu; tupate ngano, kwa sababu ya njaa.
4 Tena walikuwako wengine waliosema, Tumekopa fedha ili kulipa kodi ya mfalme kwa kuweka rehani mashamba yetu, na mizabibu yetu.
5 Walakini miili yetu ni kama miili ya ndugu zetu, na watoto wetu kama watoto wao; kumbe! Mnawatia utumwani wana wetu na binti zetu kuwa watumishi, na baadhi ya binti zetu wamekwisha kutiwa utumwani; wala hatuwezi kujiepusha na hayo; maana watu wengine wana mashamba yetu na mizabibu yetu.
6 Nami nilikasirika sana, niliposikia kilio chao, na maneno hayo.
7 Ndipo nikafanya shauri na nafsi yangu, nikagombana na wakuu na maofisa, nikawaambia, Nyote mnatoza watu riba, mtu na ndugu yake. Nikakutanisha mkutano mkubwa ili kukabiliana nao.
8 Nikawaambia, Sisi kwa kadiri ya uwezo wetu tumewakomboa ndugu zetu Wayahudi, waliouzwa kwa makafiri; na ninyi mnataka kuwauza ndugu zenu, tena kuwauza ili sisi tuwanunue? Wakanyamaza kimya, wasiweze kusema neno lolote.
9 Tena nilisema, Neno hili mnalolitenda si jema; je! Haiwapasi ninyi kwenda katika kicho cha Mungu wetu, kwa sababu ya mashutumu ya makafiri adui zetu?
10 Isitoshe mimi, ndugu zangu na watumishi wangu, tunawakopesha fedha na ngano ili kujipatia faida? Tafadhali na tuliache jambo hili la riba.
11 Naomba, warudishieni hivi leo mashamba yao, mashamba yao ya mizabibu, mashamba yao ya mizeituni, nyumba zao, lile fungu la mia la fedha, la ngano, la divai, na la mafuta, mnalowatoza.
12 Ndipo wakasema, Tutawarudishia, wala hatutataka kitu kwao; tutafanya hivyo, kama ulivyosema. Kisha nikawaita makuhani, nikawaapisha, ya kwamba watafanya kama walivyoahidi.
13 Tena nikakung’uta nguo yangu, nikasema, Mungu na amkung’ute vivyo hivyo kila mtu nyumbani mwake, na kazini mwake, asiyeitimiza ahadi hiyo; naam, na akung’utwe vivyo hivyo, na kuwa hana kitu. Mkutano wote wakasema, Amina; wakamhimidi BWANA. Nao watu wakafanya kama walivyoahidi.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *