Biblia inasema nini kuhusu Reubeni – Mistari yote ya Biblia kuhusu Reubeni

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Reubeni

Mwanzo 29 : 32
32 Lea akapata mimba akazaa mwana, akampa jina lake, Reubeni, maana alisema, Kwa kuwa BWANA ameona mateso yangu; sasa mume wangu atanipenda.

1 Mambo ya Nyakati 2 : 1
1 ② Hawa ndio wana wa Israeli; Reubeni, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni;

Mwanzo 30 : 14
14 Reubeni akaenda siku za mavuno ya ngano akaona tunguja shambani, akazileta kwa Lea mamaye. Ndipo Raheli akamwambia Lea, Nipe mimi baadhi ya tunguja za mwanao.

Mwanzo 35 : 22
22 Ikawa Israeli alipokuwa akikaa katika nchi ile, Reubeni akaenda akalala na Bilha, suria wa babaye; Israeli akasikia habari. Basi hao wana wa Yakobo walikuwa kumi na wawili.

Mwanzo 49 : 4
4 Umekuwa kama maji yavukavyo mpaka, basi nawe hutafana tena, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.

1 Mambo ya Nyakati 5 : 1
1 Na wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; (kwa maana ndiye aliyekuwa mzaliwa wa kwanza, lakini, kwa kuwa alikinajisi kitanda cha babaye, haki yake ya mzaliwa wa kwanza walipewa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli; tena nasaba isihesabiwe kwa kuifuata hiyo haki ya mzaliwa wa kwanza.

Mwanzo 37 : 30
30 ⑭ Akarudi kwa ndugu zake, akasema, Mtoto hayuko, nami niende wapi?

Mwanzo 42 : 22
22 ⑪ Reubeni akajibu, akawaambia, Sikuwaambia, nikisema, Msimkosee kijana? Wala hamkusikia; kwa hiyo tunadaiwa damu yake.

Mwanzo 42 : 37
37 Reubeni akamwambia baba yake, akasema, Uwaue wanangu wawili nisipomrudisha kwako; mtie katika mikono yangu, nami nitamrudisha kwako.

Mwanzo 49 : 4
4 Umekuwa kama maji yavukavyo mpaka, basi nawe hutafana tena, Kwa sababu ulikipanda kitanda cha baba yako, Ukakitia unajisi; alikipandia kitanda changu.

Mwanzo 46 : 9
9 Na wana wa Reubeni; Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi.

Kutoka 6 : 14
14 Hawa ndio vichwa vya nyumba za baba zao: wana wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa Israeli; ni Hanoki, na Palu, na Hesroni, na Karmi; hao ni jamaa za Reubeni.

1 Mambo ya Nyakati 5 : 6
6 na mwanawe huyo ni Beera, ambaye Tiglath-Pileseri, mfalme wa Ashuru, alimchukua mateka; ndiye aliyekuwa mkuu wa Wareubeni.

Hesabu 16 : 1
1 Basi Kora, mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, akatwaa watu, pamoja na Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni, mwana wa Pelethi, waliokuwa wana wa Reubeni;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *