Biblia inasema nini kuhusu Rehoboamu – Mistari yote ya Biblia kuhusu Rehoboamu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Rehoboamu

1 Wafalme 11 : 43
43 Naye Sulemani akalala na baba zake, akazikwa katika mji wa Daudi baba yake; na Rehoboamu mwanawe akatawala mahali pake.

2 Mambo ya Nyakati 9 : 31
31 Naye Sulemani akalala na baba zake, akazikwa mjini mwa Daudi babaye; Rehoboamu mwanawe akatawala badala yake.

1 Wafalme 12 : 15
15 Basi mfalme hakuwasikia wale watu; maana jambo hili lilitoka kwa BWANA, ili alitimize neno lake, BWANA alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa kinywa cha Ahiya Mshiloni.

2 Mambo ya Nyakati 10 : 15
15 Basi mfalme hakuwasikia watu wale; maana jambo hili lilitoka kwa Mungu, ili alithibitishe neno lake alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa mkono wa Ahiya Mshiloni.

1 Wafalme 12 : 24
24 BWANA asema hivi, Msiende, wala msipigane na ndugu zenu wana wa Israeli; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi, wakalisikiliza neno la BWANA, wakarudi, wakaenda zao, sawasawa na neno la BWANA.

2 Mambo ya Nyakati 10 : 19
19 Hivyo Israeli wakaasi juu ya nyumba ya Daudi, hata leo.

2 Mambo ya Nyakati 11 : 4
4 BWANA asema hivi, Hamtapanda wala kupigana na ndugu zenu; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi wakayatii maneno ya BWANA wakarudi wasiende kupigana na Yeroboamu.

2 Mambo ya Nyakati 11 : 23
23 Akafanya kwa akili, akawatawanya wanawe wote kati ya nchi zote za Yuda na Benyamini, katika kila mji wenye boma; akawapa vyakula tele. Akawatafutia wake wengi.

1 Wafalme 14 : 28
28 Ikawa kila wakati mfalme alipoingia nyumbani mwa BWANA, hao walinzi walizichukua; wakazirudisha tena katika chumba cha walinzi.

2 Mambo ya Nyakati 12 : 12
12 ① Naye alipojinyenyekeza, ghadhabu ya BWANA ikamgeukia mbali, asimharibu kabisa; tena yalionekana katika Yuda mambo mema.

1 Wafalme 14 : 31
31 Rehoboamu akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze mjini mwa Daudi. Na jina la mamaye aliitwa Naama, Mwamoni. Na mwanawe, Abiya,[21] alitawala mahali pake.

2 Mambo ya Nyakati 12 : 16
16 Rehoboamu akalala na babaze, akazikwa katika mji wa Daudi. Na Abiya mwanawe alitawala mahali pake.

Mathayo 1 : 7
7 Sulemani akamzaa Rehoboamu; Rehoboamu akamzaa Abiya; Abiya akamzaa Asa;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *