Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Refaya
1 Mambo ya Nyakati 3 : 21
21 Na wana wa Hanania; Pelatia na Yeshaya; na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania.[1]
1 Mambo ya Nyakati 4 : 42
42 Na baadhi yao, wana wa Simeoni wapatao watu mia tano, wakaenda mpaka mlima Seiri, na majemadari wao walikuwa Pelatia, na Nearia, na Refaya, na Uzieli, wana wa Ishi.
1 Mambo ya Nyakati 7 : 2
2 Na wana wa Tola; Uzi, na Refaya, na Yerieli, na Yamai, na Ibsamu, na Shemueli, wakuu wa koo za baba zao, yaani, wa Tola; watu hodari wa vita katika vizazi vyao; hesabu yao katika siku za Daudi ilikuwa watu elfu ishirini na mbili na mia sita.
1 Mambo ya Nyakati 9 : 43
43 na Mosa akamzaa Binea; na mwanawe huyo alikuwa Refaya, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli;
1 Mambo ya Nyakati 8 : 37
37 na Mosa akamzaa Binea; na mwanawe huyo alikuwa Refaya, na mwanawe huyo ni Ekasa, na mwanawe huyo ni Aseli;
Nehemia 3 : 9
9 Na baada yao Refaya, mwana wa Huri akajenga, mtawala[3] wa nusu ya Yerusalemu.
Leave a Reply