Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Raheli
Mwanzo 29 : 12
12 Yakobo akamwarifu Raheli ya kuwa yeye ni ndugu wa babaye, na ya kuwa ni mwana wa Rebeka. Basi akapiga mbio akampasha babaye habari.
Mwanzo 29 : 30
30 Ndipo Yakobo[14] akaingia kwa Raheli, akampenda Raheli kuliko Lea, akatumika kwa ajili yake miaka saba mingine.
Mwanzo 29 : 31
31 BWANA akaona ya kwamba Lea hakupendwa, naye akafungua tumbo lake; bali Raheli alikuwa hazai.
Mwanzo 30 : 8
8 Raheli akasema, Kwa mashindano makuu nimeshindana na dada yangu, nikashinda. Akamwita jina lake Naftali.
Mwanzo 30 : 15
15 Naye akamwambia, Je, Ni jambo dogo kuninyang’anya mume wangu; hata wataka kuzitwaa tunguja za mwanangu pia? Raheli akamwambia, Kwa hiyo atalala kwako usiku huu kwa tunguja za mwanao.
Mwanzo 30 : 34
34 Labani akasema, Tazama, na iwe hivi kama usemavyo.
Mwanzo 30 : 25
25 Ikawa Raheli alipomzaa Yusufu, Yakobo akamwambia Labani, Nipe ruhusa niende kwetu, na kwenye nchi yangu.
Mwanzo 35 : 18
18 Ikawa hapo katika kutoa roho yake, maana alikufa, akamwita jina lake Benoni, lakini babaye alimwita Benyamini.
Mwanzo 35 : 24
24 Wana wa Raheli, ni Yusufu na Benyamini.
Mwanzo 31 : 4
4 Yakobo akatuma watu ili kuwaita Raheli na Lea waje malishoni kwenye mifugo wake. Akawaambia,
Mwanzo 31 : 19
19 Basi Labani alikuwa amekwenda kuwakata manyoya kondoo zake, na Raheli akaviiba vinyago vya babaye.
Mwanzo 31 : 35
35 Naye Raheli akamwambia babaye, Bwana wangu asikasirike kwa sababu siwezi kuinuka mbele yako, maana nimeshikwa na mambo ya kike. Akatafuta, wala hakuviona vile vinyago.
Mwanzo 35 : 20
20 ⑳ Yakobo akasimamisha nguzo juu ya kaburi lake, ndiyo nguzo ya kaburi la Raheli hata leo.
Mwanzo 48 : 7
7 Na mimi nilipokuja kutoka Padan, Raheli akanifia katika nchi ya Kanaani, njiani, si mwendo mkubwa kabla ya kufika Efrata. Nikamzika katika njia ya Efrata, ndio Bethlehemu.
Leave a Reply