Biblia inasema nini kuhusu Rafa – Mistari yote ya Biblia kuhusu Rafa

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Rafa

1 Mambo ya Nyakati 8 : 2
2 na wa nne Noha, na wa tano Rafa.

1 Mambo ya Nyakati 8 : 37
37 na Mosa akamzaa Binea; na mwanawe huyo alikuwa Refaya, na mwanawe huyo ni Ekasa, na mwanawe huyo ni Aseli;

1 Mambo ya Nyakati 9 : 43
43 na Mosa akamzaa Binea; na mwanawe huyo alikuwa Refaya, na mwanawe huyo ni Eleasa, na mwanawe huyo ni Aseli;

2 Samweli 21 : 16
16 Naye Ishi-benobu, aliyekuwa mmoja wa Warefai,[14] ambaye uzito wa mkuki wake ulikuwa shekeli mia tatu za shaba kwa uzani, naye amejifungia upanga mpya, alijaribu kumwua Daudi.

2 Samweli 21 : 20
20 Kulikuwa na vita tena huko Gathi; ambako kulikuwa na mtu mrefu sana, mwenye vidole sita katika kila mkono, na vidole sita katika kila mguu, jumla yake ishirini na vinne; yeye naye alizaliwa kwa Mrefai.

2 Samweli 21 : 22
22 Hao wanne walizaliwa kwake huyo Mrefai wa Gathi; wakaanguka kwa mkono wa Daudi, na kwa mikono ya watumishi wake.

1 Mambo ya Nyakati 20 : 4
4 Ikawa baada ya hayo, kulitokea vita na Wafilisti huko Gezeri; ndipo Sibekai, Mhushathi, alipomwua Safu, mmojawapo wa Warefai;[14] nao Wafilisti[15] wakashindwa.

1 Mambo ya Nyakati 20 : 6
6 Kulikuwa na vita tena huko Gathi; ambapo palikuwa na mtu mrefu sana, mwenye vidole vya mikono na miguu ishirini na vinne, kila mguu sita, na kila mkono sita; naye alizaliwa na Mrefai.[17]

1 Mambo ya Nyakati 20 : 8
8 Hao walizaliwa kwake huyo Mrefai[18] wa Gathi, nao wakaanguka kwa mkono wa Daudi, na kwa mkono wa watumishi wake.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *