Biblia inasema nini kuhusu Punda – Mistari yote ya Biblia kuhusu Punda

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Punda

Mwanzo 12 : 16
16 Naye akamtendea Abramu mema kwa ajili yake; naye alikuwa na kondoo na ng’ombe, na punda dume, na watumwa, na wajakazi, na punda majike, na ngamia.

Mwanzo 24 : 35
35 na BWANA amembarikia sana bwana wangu, amekuwa mtu mkuu; amempa kondoo, na ng’ombe, na fedha, na dhahabu, na watumishi, na wajakazi, na ngamia, na punda.

Mwanzo 32 : 5
5 ④ nami nina ng’ombe, na punda, na kondoo, na watumwa, na vijakazi; nami nimepeleka watu nimpashe bwana wangu habari, nipate neema machoni pako.

Mwanzo 34 : 28
28 Wakachukua kondoo wao, na ng’ombe wao, na punda wao, na vitu vilivyokuwamo mjini, na vile vilivyokuwako kondeni.

Hesabu 31 : 34
34 na punda elfu sitini na moja,

Hesabu 31 : 45
45 na punda elfu thelathini, na mia tano,

1 Mambo ya Nyakati 5 : 21
21 Wakateka nyara ng’ombe wao, na ngamia wao elfu hamsini, na kondoo wao elfu mia mbili na hamsini, na punda wao elfu mbili; na watu elfu mia moja.

Ezra 2 : 67
67 ngamia wao, mia nne thelathini na watano; punda wao elfu sita, mia saba na ishirini.

Nehemia 7 : 69
69 ngamia wao, mia nne thelathini na watano; punda zao, elfu sita na mia saba na ishirini.

Mwanzo 22 : 3
3 Abrahamu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu.

Hesabu 22 : 33
33 punda akaniona, akageuka upande mbele zangu mara tatu hizi; kama asingejiepusha nami, bila shaka ningalikuua wewe, nikamwacha yeye hai.

Yoshua 15 : 18
18 Kisha ikawa, hapo huyo mwanamke alipokwenda kwa mumewe, akamtaka aombe shamba kwa baba yake; akashuka katika punda wake; Kalebu akamwuliza, Unataka nikupe nini?

Waamuzi 1 : 14
14 Ikawa hapo alipokwenda kukaa naye, huyo mwanamke akamtaka ili aombe shamba kwa baba yake; na huyo mwanamke akashuka katika punda wake; Kalebu akamwuliza, Una haja gani utakayo?

Waamuzi 5 : 10
10 ⑧ Itangazeni habari, ninyi mpandao punda weupe, Ninyi mketio juu ya mazulia ya thamani, Na ninyi mnaopita njiani kwa miguu.

1 Samweli 25 : 23
23 ⑤ Ndipo hapo Abigaili alipomwona Daudi, alifanya haraka kushuka juu ya punda wake, akamwangukia Daudi kifudifudi, akainama mpaka chini.

2 Mambo ya Nyakati 28 : 15
15 Wakaondoka wale watu waliotajwa majina yao, wakawatwaa wafungwa, wakawavika kwa zile nyara wale wote waliokuwa uchi, wakawapa mavazi na viatu, wakawalisha, wakawanywesha, wakawatia mafuta, wakawapandisha waliokuwa dhaifu miongoni mwao juu ya punda wakawaleta Yeriko, mji wa mitende, kwa ndugu zao; kisha wakarudi Samaria.

Zekaria 9 : 9
9 ⑫ Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwanapunda, mtoto wa punda.

Mathayo 21 : 2
2 Nendeni katika kijiji kile kinachowakabili, na mara mtaona punda amefungwa, na mwanapunda pamoja naye; wafungueni mniletee.

Mathayo 21 : 5
5 ⑦ Mwambieni binti Sayuni Tazama, mfalme wako anakuja kwako, Mpole, naye amepanda punda, Na mwanapunda, mtoto wa punda.

Luka 13 : 15
15 Lakini Bwana akajibu akasema, Enyi wanafiki, kila mmoja wenu, je! Hamfungui ng’ombe wake au punda wake siku ya sabato katika zizi, aende naye kumnywesha?

Yohana 12 : 15
15 Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwanapunda.

Zekaria 9 : 9
9 ⑫ Furahi sana, Ee binti Sayuni; Piga kelele, Ee binti Yerusalemu; Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwanapunda, mtoto wa punda.

Mwanzo 42 : 26
26 Wakawatwika punda wao nafaka yao, wakatoka huko.

2 Samweli 16 : 1
1 Naye Daudi alipokipita punde hicho kilele cha mlima, tazama, Siba, mtumwa wa Mefiboshethi, akamkuta, na punda wawili waliotandikwa, na juu yao mikate mia mbili ya ngano, na vishada mia moja vya zabibu kavu, na matunda mia moja ya wakati wa joto, na kiriba cha divai.

Isaya 30 : 6
6 Ufunuo juu ya wanyama wa Negebu. Katikati ya nchi ya taabu na dhiki, Ambayo hutoka huko simba jike na simba angurumaye, Nyoka na joka la moto arukaye, Huchukua mali zao mabegani mwa punda wachanga, Na hazina zao juu ya nundu za ngamia Waende kwa watu ambao hawatawafaa kitu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *