Biblia inasema nini kuhusu Pumzi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Pumzi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Pumzi

Mwanzo 2 : 7
7 BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa kiumbe hai.

Mwanzo 7 : 22
22 ⑱ kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu.

Matendo 17 : 25
25 ⑭ wala hatumikiwi kwa mikono ya wanadamu kana kwamba anahitaji kitu chochote; kwa maana ndiye anayewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.

2 Samweli 22 : 16
16 Ndipo ilipoonekana mikondo ya bahari, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Kwa kukemea kwake BWANA, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwake.

Ayubu 4 : 9
9 Kwa pumzi za Mungu huangamia. Na kwa kuvuma kwa hasira zake humalizika.

Ayubu 15 : 30
30 ⑱ Hataondoka gizani; Ndimi za moto zitayakausha matawi yake, Naye ataondoka kwa pumzi za kinywa chake.

Ayubu 33 : 4
4 Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.

Ayubu 37 : 10
10 Kwa pumzi ya Mungu barafu hutokea; Na uso wa maji huganda punde.

Zaburi 18 : 15
15 Ndipo ilipoonekana mikondo ya maji, Misingi ya ulimwengu ikafichuliwa, Ee BWANA, kwa kukemea kwako, Kwa mvumo wa pumzi ya puani mwako.

Zaburi 33 : 6
6 Kwa neno la BWANA mbingu ziliumbwa, Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake.

Isaya 30 : 33
33 Maana Tofethi imewekwa tayari tokea zamani, naam, imewekwa tayari kwa mfalme huyo; ameifanya kubwa, inakwenda chini sana; tanuri yake ni moto na kuni nyingi; pumzi ya BWANA, kama mto wa kiberiti, huiwasha.

Ezekieli 37 : 9
9 Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapulizie hawa waliouawa, wapate kuishi.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *