Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia pumzi
Ayubu 33 : 4
4 Roho ya Mungu imeniumba, Na pumzi za Mwenyezi hunipa uhai.
Mwanzo 2 : 7
7 BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa kiumbe hai.
2 Timotheo 3 : 16
16 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki;
Ayubu 27 : 3
3 (Kwa kuwa uhai wangu ungali mzima ndani yangu, Na Roho ya Mungu iko katika pua yangu;)
Yohana 20 : 22
22 Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu.
Ayubu 34 : 14 – 15
14 ⑯ Kama akimwekea mtu moyo wake, Akijikusanyia roho yake na pumzi zake;
15 Wenye mwili wote wangeangamia pamoja, Nao wanadamu watarejea tena kuwa mavumbi.
Ezekieli 37 : 9
9 Ndipo akaniambia, Tabiri, utabirie upepo, mwanadamu, ukauambie upepo, Bwana MUNGU asema hivi; Njoo, kutoka pande za pepo nne, Ee pumzi, ukawapulizie hawa waliouawa, wapate kuishi.
Isaya 42 : 5
5 ⑮ Mungu BWANA anena, yeye aliyeziumba mbingu, na kuzitanda; yeye aliyeitandaza nchi na mazao yake; yeye awapaye pumzi watu walio juu yake; yeye awapaye roho wao waendao ndani yake.
Leave a Reply