Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia pombe
Waefeso 5 : 18
18 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;
Mithali 20 : 1
1 ③ Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima.
Mithali 23 : 29 – 35
29 Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu?
30 Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika.
31 Usiutazame mvinyo iwapo ni mwekundu; uitiapo bilauri rangi yake, ushukapo taratibu;
32 Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira.
33 Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka.
34 Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti.
35 Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.
Warumi 14 : 21
21 Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lolote ambalo kwa hilo ndugu yako hukwazwa.
Isaya 5 : 22
22 Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, na walio hodari wa kuchanganya vileo;
Mhubiri 9 : 7
7 Wewe nenda zako, ule chakula chako kwa furaha, unywe mvinyo yako kwa moyo wa kuchangamka; kwa kuwa Mungu amekwisha kuzikubali kazi zako.
1 Timotheo 5 : 23
23 Tokea sasa usinywe maji tu lakini tumia mvinyo kidogo, kwa ajili ya tumbo lako, na magonjwa yakupatayo mara kwa mara.
Mambo ya Walawi 10 : 9
9 Usinywe divai wala kileo chochote, wewe, wala wanao pamoja nawe, hapo mwingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba msife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu;
Isaya 5 : 11
11 ⑰ Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hadi usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao!
1 Timotheo 3 : 8
8 ⑦ Vivyo hivyo mashemasi[3] na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana, si watu wanaotamani fedha ya aibu;
Wagalatia 5 : 19 – 21
19 ⑬ Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi,
20 ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, mafarakano, uzushi,
21 ⑭ husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Zaburi 104 : 14 – 15
14 Huyameesha majani kwa makundi, Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu; Ili atoe chakula katika nchi,
15 Na divai imfurahishe mtu moyo wake. Aung’aze uso wake kwa mafuta, Na mkate umburudishe mtu moyo wake.
Mathayo 11 : 18 – 19
18 Maana Yohana alikuja, hali wala hanywi, wakasema, Ana pepo.
19 Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakasema, Mlafi huyu, na mlevi, rafiki yao watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imejulikana kuwa ina haki kwa kazi zake.
Mithali 31 : 6
6 Mpe kileo yeye aliye karibu na kupotea; Kampe divai yeye aliye na uchungu nafsini.
Luka 7 : 34
34 Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa; nanyi mwasema, Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi.
Hosea 4 : 11
11 ② Uzinzi na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu.
Warumi 13 : 13
13 ⑧ Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu.
Hesabu 6 : 3
3 atajitenga na divai na vileo; hatakunywa siki ya divai, wala siki ya kileo, wala asinywe maji yoyote ya zabibu, wala asile zabibu, mbichi wala zilizokauka.
Wagalatia 5 : 21
21 ⑭ husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu.
Mithali 23 : 20 – 21
20 Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; Miongoni mwao walao nyama kwa pupa.
21 Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.
Leave a Reply