Biblia inasema nini kuhusu Pilato, Pontio – Mistari yote ya Biblia kuhusu Pilato, Pontio

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Pilato, Pontio

Mathayo 27 : 2
2 wakamfunga, wakamchukua, wakampeleka kwa Pilato aliyekuwa mtawala.

Luka 3 : 1
1 Mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alipokuwa mtawala wa Yudea, na Herode mfalme wa Galilaya, na Filipo, ndugu yake, mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania mfalme wa Abilene,

Luka 13 : 1
1 Na wakati uo huo walikuwapo watu waliompasha habari ya Wagalilaya wale ambao Pilato alichanganya damu yao na dhabihu zao.

Yohana 18 : 40
40 Basi wakapiga kelele tena kusema, Si huyu, bali Baraba. Naye yule Baraba alikuwa mnyang’anyi.

Matendo 3 : 13
13 Mungu wa Abrahamu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake Yesu, ambaye ninyi mlimsaliti na kumkana mbele ya Pilato, alipokuwa ametoa hukumu yake afunguliwe.

Matendo 4 : 27
27 ⑧ Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,

Matendo 13 : 28
28 Na ijapokuwa hawakuona sababu ya kumwua wakamwomba Pilato auawe.

1 Timotheo 6 : 13
13 Nakuagiza mbele za Mungu anayevihifadhi hai vitu vyote, na mbele za Kristo Yesu, aliyeyaungama maungamo mazuri yale mbele ya Pontio Pilato,

Mathayo 27 : 58
58 mtu huyu alimwendea Pilato akaomba apewe mwili wa Yesu. Ndipo Pilato akaamuru apewe.

Marko 15 : 45
45 Hata alipokwisha kupata hakika kutoka kwa yule kamanda, alimpa Yusufu yule maiti.

Luka 23 : 52
52 mtu huyo alikwenda kwa Pilato, akataka kupewa mwili wa Yesu.

Yohana 19 : 38
38 Hata baada ya hayo Yusufu wa Arimathaya, naye ni mwanafunzi wa Yesu, (lakini kwa siri, kwa hofu ya Wayahudi), alimwomba Pilato ruhusa ili auondoe mwili wake Yesu. Na Pilato akampa ruhusa. Basi akaenda, akauondoa mwili wake.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *