Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Phut
Mwanzo 10 : 6
6 Na wana wa Hamu ni Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani.
1 Mambo ya Nyakati 1 : 8
8 Wana wa Hamu; Kushi, na Misri, na Putu, na Kanaani.
Ezekieli 27 : 10
10 Watu wa Uajemi na Ludi na Putu walikuwa katika jeshi lako, watu wako wa vita; walitungika ngao na chapeo ndani yako; wakadhihirisha uzuri wako.
Nahumu 3 : 9
9 Kushi na Misri walikuwa nguvu zake, nazo zilikuwa hazina mpaka; Puti na Walibya walikuwa wasaidizi wake.
Yeremia 46 : 9
9 Haya! Pandeni, enyi farasi; Jihimizeni, enyi magari ya vita; Mashujaa nao na watoke nje Kushi na Puti, watumiao ngao; Nao Waludi, washikao uta na kuupinda.
Ezekieli 30 : 5
5 ⑦ Kushi, na Putu, na Ludi, na watu wote waliochanganyika, na Kubu, na wana wa nchi ya agano, wataanguka kwa upanga pamoja nao.
Ezekieli 38 : 5
5 Uajemi, na Kushi, na Putu, pamoja nao; wote wana ngao na chapeo;
Leave a Reply