Biblia inasema nini kuhusu Pentekoste – Mistari yote ya Biblia kuhusu Pentekoste

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Pentekoste

Kutoka 34 : 22
22 Nawe utaitunza sikukuu ya majuma,[40] nayo ni ya malimbuko ya mavuno ya ngano, na sikukuu ya kukusanya vitu mwisho wa mwaka.

Kumbukumbu la Torati 16 : 10
10 Nawe sikukuu ya majuma umfanyie BWANA, Mungu wako, kwa kutoa sadaka ya hiari ya mkono wako, utakayotoa kwa kadiri akubarikiavyo BWANA, Mungu wako;

Kutoka 23 : 16
16 tena, sikukuu ya mavuno,[25] hayo malimbuko ya kazi zako za kupanda mashambani; tena, sikukuu ya kukusanya, mwisho wa mwaka, hapo utakapokusanya hayo uliyoyataabikia shambani.

Hesabu 28 : 26
26 ⑩ Tena katika siku ya malimbuko, hapo mtakapomsogezea BWANA sadaka ya unga mpya katika sikukuu yenu ya majuma mtakuwa na kusanyiko takatifu; hamtafanya kazi yoyote ya utumishi;

Matendo 2 : 1
1 Wakati ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwako wote mahali pamoja.

Matendo 20 : 16
16 ⑬ Kwa sababu Paulo alikusudia kusafiri pasipo kupitia Efeso merikebuni, asije akakawia katika Asia; kwa maana alikuwa na haraka, akitaka kuwahi Yerusalemu siku ya Pentekoste, kama ikiwezekana.

1 Wakorintho 16 : 8
8 ③ Lakini nitakaa Efeso hadi siku ya Pentekoste; ④

Kutoka 23 : 16
16 tena, sikukuu ya mavuno,[25] hayo malimbuko ya kazi zako za kupanda mashambani; tena, sikukuu ya kukusanya, mwisho wa mwaka, hapo utakapokusanya hayo uliyoyataabikia shambani.

Kutoka 34 : 22
22 Nawe utaitunza sikukuu ya majuma,[40] nayo ni ya malimbuko ya mavuno ya ngano, na sikukuu ya kukusanya vitu mwisho wa mwaka.

Mambo ya Walawi 23 : 21
21 Nanyi mtatangaza suku iyo hiyo; kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; msifanye kazi yoyote ya utumishi; ni amri ya milele katika makao yenu yote, katika vizazi vyenu.

Hesabu 28 : 31
31 Zaidi ya hiyo sadaka ya kuteketezwa ya sikuzote, na sadaka yake ya unga, mtasongeza wanyama hao (watakuwa wakamilifu kwenu), pamoja na sadaka zake za vinywaji.

Kumbukumbu la Torati 16 : 12
12 Nawe kumbuka kwamba ulikuwa mtumwa huko Misri; tena zishike amri hizi kwa kuzifanya.

Kumbukumbu la Torati 16 : 16
16 Mara tatu kwa mwaka na watokee wana wa kiume wako wote mbele za BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua; katika sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu, na katika sikukuu ya majuma, na katika sikukuu ya vibanda; wala wasitokee mbele za BWANA mikono mitupu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *