Biblia inasema nini kuhusu Peka – Mistari yote ya Biblia kuhusu Peka

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Peka

2 Wafalme 15 : 25
25 Na Peka mwana wa Remalia, jemadari wake, akamfanyia uhaini, akampiga huko Samaria, katika ngome ya nyumba ya mfalme, pamoja na Argobu na Arie; na pamoja naye walikuwako watu hamsini wa Wagileadi. Akamwua, akatawala mahali pake.

2 Wafalme 15 : 27
27 Katika mwaka wa hamsini na mbili wa Uzia mfalme wa Yuda Peka mwana wa Remalia alianza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; akatawala miaka ishirini.

2 Mambo ya Nyakati 28 : 6
6 Peka mwana wa Remalia akawaua katika Yuda siku moja watu elfu mia moja na ishirini, mashujaa wote; kwa sababu walikuwa wamemwacha BWANA, Mungu wa baba zao.

2 Wafalme 15 : 31
31 Basi mambo yote ya Peka yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, tazama, yameandikwa katika Iitabu cha Kumbukumbu cha Wafalme wa Israeli.

Isaya 7 : 16
16 Kwa maana kabla mtoto huyo hajajua kuyakataa mabaya na kuyachagua mema, nchi ile, ambayo wewe unawachukia wafalme wake wawili, itaachwa ukiwa.

Isaya 8 : 10
10 Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *