Biblia inasema nini kuhusu Pazia – Mistari yote ya Biblia kuhusu Pazia

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Pazia

Waraka kwa Waebrania 6 : 19
19 tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia,

Waraka kwa Waebrania 9 : 3
3 Na nyuma ya pazia la pili, ile hema iitwayo Patakatifu pa patakatifu,

Kutoka 26 : 33
33 ⑦ Nawe tungika lile pazia chini ya vile vifungo, nawe lete lile sanduku la ushuhuda na kulitia humo nyuma ya pazia; na lile pazia litawagawanyia kati ya patakatifu, na mahali patakatifu sana.

Kutoka 36 : 36
36 Naye akafanya kwa ajili yake nguzo nne za mti wa mshita, akazifunika dhahabu; na kulabu zake zilikuwa za dhahabu; naye akasubu kwa ajili yake vitako vinne vya fedha.

Kutoka 35 : 12
12 hilo sanduku, miti yake, hicho kiti cha rehema na lile pazia la sitara;

Kutoka 39 : 34
34 na kifuniko chake cha ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu, na kifuniko cha ngozi za pomboo, na pazia la sitara;

Kutoka 40 : 21
21 kisha akalileta sanduku akalitia ndani ya maskani, naye akalitundika pazia la sitara, akalisitiri sanduku la ushuhuda; kama BWANA alivyomwamuru Musa.

Hesabu 4 : 5
5 ① hapo watakapoanza safari, Haruni ataingia ndani, na wanawe, nao watalishusha pazia la sitara, na kulifunika sanduku la ushahidi[4] kwa hilo pazia;

2 Mambo ya Nyakati 3 : 14
14 ⑧ Akalifanya pazia la samawati na urujuani na nyekundu, na kitani safi, akaitengeneza makerubi.

Mathayo 27 : 51
51 ⑬ Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hadi chini; nchi ikatetemeka; miamba ikapasuka;

Marko 15 : 38
38 Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hadi chini.

Luka 23 : 45
45 ⑧ jua limepungua nuru yake; pazia la hekalu likapasuka katikati.

Waraka kwa Waebrania 10 : 20
20 ⑥ njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake;

Mwanzo 24 : 65
65 ⑩ Akamwambia mtumishi, Ni nani mtu huyu ajaye shambani kutulaki? Mtumishi akasema, Huyu ndiye bwana wangu. Basi akatwaa shela yake akajifunika.

Mwanzo 38 : 14
14 Basi akavua nguo za ujane wake, akajivika utaji, akajifunika uso, akakaa mlangoni pa Enaimu, karibu na njia ya kuendea Timna. Maana aliona ya kwamba Shela amekuwa mtu mzima, ijapokuwa hakuozwa awe mkewe.

Mwanzo 38 : 19
19 Akaondoka, akaenda zake, akavua utaji wake, na kuvaa mavazi ya ujane wake.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *