Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Pauni
1 Wafalme 10 : 17
17 Na vigao mia tatu vya dhahabu iliyofuliwa; kila kigao kimoja kilipata mane tatu za dhahabu. Mfalme akaviweka katika nyumba ya msitu wa Lebanoni.
Ezra 2 : 69
69 wakatoa kadiri walivyoweza, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni[6] za dhahabu elfu sitini na moja, na mane[7] za fedha elfu tano, na mavazi mia moja ya makuhani.
Nehemia 7 : 72
72 Na mabaki ya watu wakatoa darkoni za dhahabu elfu ishirini, na mane za fedha elfu mbili, na mavazi ya makuhani sitini na saba.
Yohana 12 : 3
3 Basi Mariamu akatwaa ratili ya marhamu ya nardo safi yenye thamani nyingi, akampaka Yesu miguu, akamfuta miguu kwa nywele zake. Nayo nyumba pia ikajaa harufu ya marhamu.
Leave a Reply