Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Patakatifu
Waraka kwa Waebrania 9 : 2
2 Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate mitakatifu; ndipo palipoitwa, Patakatifu.
Kutoka 25 : 8
8 Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao.
Mambo ya Walawi 19 : 30
30 Zishikeni Sabato zangu, mpaheshimu patakatifu pangu; mimi ndimi BWANA.
Mambo ya Walawi 26 : 2
2 Zishikeni Sabato zangu, na kupastahi patakatifu pangu; mimi ndimi BWANA.
Kutoka 27 : 21
21 ⑳ Ndani ya ile hema ya kukutania, nje ya hilo pazia, lililo mbele ya huo ushuhuda, Haruni na wanawe wataitengeza tangu jioni hadi asubuhi mbele ya BWANA; itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyao vyote kwa ajili ya wana wa Israeli.
Mambo ya Walawi 24 : 3
3 Hapo nje ya pazia la ushahidi, ndani ya hema ya kukutania, Haruni ataitengeneza tangu jioni hadi asubuhi mbele za BWANA daima; ni amri ya milele katika vizazi vyenu.
Hesabu 18 : 5
5 Nanyi mtahudumu katika patakatifu na huduma ya madhabahuni, isiwe ghadhabu juu ya wana wa Israeli tena.
Maombolezo 2 : 7
7 Bwana ameitupilia mbali madhabahu yake, Amepachukia patakatifu pake; Amezitia katika mikono ya hao adui Kuta za majumba yake; Wamepiga kelele ndani ya nyumba ya BWANA Kama katika sikukuu.
Maombolezo 2 : 20
20 ⑩ Tazama, BWANA, uangalie, Ni nani uliyemtenda hayo! Je! Wanawake wale mazao yao, Watoto waliowabeba? Je! Kuhani na nabii wauawe Katika patakatifu pa Bwana?
Ezekieli 42 : 20
20 Alipima pande zake zote nne; lilikuwa na ukuta pande zote, urefu wake mianzi mia tano, na upana wake mianzi mia tano, ili kupatenga mahali palipo patakatifu, na mahali ambapo ni pa watu wote.
Ezekieli 11 : 16
16 ⑱ basi nena, Bwana MUNGU asema hivi, Ikiwa mimi nimewahamisha, wakae katika mataifa, na ikiwa mimi nimewatawanya katika nchi kadha wa kadha, pamoja na hayo nitakuwa patakatifu kwao kwa muda mchache, katika nchi zile walizozifika.
Waraka kwa Waebrania 8 : 2
2 mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala si mwanadamu.
Leave a Reply