Biblia inasema nini kuhusu Parani – Mistari yote ya Biblia kuhusu Parani

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Parani

Mwanzo 21 : 21
21 ⑰ Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.

Hesabu 10 : 12
12 ⑦ Wana wa Israeli wakasafiri kwenda mbele, kwa safari zao kutoka jangwa la Sinai; na hilo wingu likakaa katika jangwa la Parani.

Hesabu 12 : 16
16 Baada ya hayo watu wakasafiri kutoka Haserothi, wakapiga kambi katika nyika ya Parani.

Hesabu 13 : 3
3 Basi Musa akawatuma kutoka nyika ya Parani kama alivyoagizwa na BWANA; wote walikuwa ni watu walio vichwa vya wana wa Israeli.

Hesabu 13 : 26
26 Wakaenda wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote wa wana wa Israeli, katika jangwa la Parani, huko Kadeshi; wakawaletea habari, wao na mkutano wote, wakawaonesha matunda ya nchi.

Kumbukumbu la Torati 1 : 1
1 Haya ndiyo maneno Musa aliyowaambia Israeli wote ng’ambo ya Yordani nyikani, katika Araba lililoelekea Sufu, kati ya Parani, na Tofeli, na Labani, na Hazerothi, na Dizahabu.

Kumbukumbu la Torati 33 : 2
2 ⑬ Akasema, BWANA alitoka Sinai, Akawajia kutoka Seiri; Aliangaza katika kilima cha Parani, Akaja Meribath-kadeshi. Upande wa mkono wake wa kulia Palikuwa na sheria ya motomoto kwao.

Habakuki 3 : 3
3 Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake.

Hesabu 12 : 16
16 Baada ya hayo watu wakasafiri kutoka Haserothi, wakapiga kambi katika nyika ya Parani.

1 Samweli 25 : 1
1 Akafa Samweli; nao Israeli wote wakakusanyika, wakamwomboleza, wakamzika nyumbani mwake huko Rama. Kisha Daudi akaondoka, akashuka mpaka nyikani mwa Maoni.

1 Wafalme 11 : 18
18 Wakaondoka katika Midiani, wakafika Parani; wakachukua pamoja nao watu toka Parani, wakafika Misri, kwa Farao mfalme wa Misri; aliyempa nyumba, akaamuru apewe vyakula, akampa mashamba.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *