Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia panga
Mathayo 26 : 52 – 54
52 Ndipo Yesu akamwambia, Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga.
53 Ama wadhani ya kuwa mimi siwezi kumsihi Baba yangu, naye ataniletea sasa hivi zaidi ya majeshi kumi na mawili ya malaika?
54 Yatatimizwaje basi maandiko, ya kwamba hivyo ndivyo vilivyopasa kujiri?
Luka 22 : 36
36 Akawaambia, Lakini sasa mwenye mfuko na auchukue, na mkoba vivyo hivyo; naye asiye na upanga, na auze joho lake akanunue.
Warumi 13 : 4
4 kwa kuwa yeye ni mtumishi wa Mungu kwako kwa ajili ya mema. Lakini ufanyapo mabaya, ogopa; kwa maana hauchukui upanga bure; kwa kuwa ni mtumishi wa Mungu, amlipizaye kisasi mtenda mabaya kwa ajili ya ghadhabu.
Zaburi 144 : 1
1 ② Na ahimidiwe BWANA, mwamba wangu, Aifundishaye mikono yangu vita, Na vidole vyangu kupigana.
1 Samweli 25 : 13
13 Kisha Daudi akawaambia watu wake, Haya! Jifungeni kila mtu upanga wake. Nao wakajifunga kila mtu upanga wake; Daudi naye akajifunga upanga wake; nao wakapanda nyuma yake Daudi, wakiwa kama watu mia nne; na watu mia mbili wakakaa na vyombo vyao.
Waamuzi 5 : 8
8 ⑦ Walichagua miungu mipya, Ndipo kulikuwa na vita malangoni; Je! Ilionekana ngao au mkuki Katika watu elfu arubaini wa Israeli?
Nehemia 4 : 17 – 18
17 Watu wale walioujenga ukuta, na wale waliochukua mizigo, walijitweka wenyewe, kila mtu alifanya kazi kwa mkono mmoja, na kwa mkono wake wa pili alishika silaha yake;
18 nao wajenzi, kila mtu alikuwa na upanga wake, umefungwa ubavuni mwake, ndivyo alivyojenga. Na yeye aliyepiga baragumu alikuwa karibu na mimi.
Leave a Reply