Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ophrah
Yoshua 18 : 23
23 na Avimu, na Para, na Ofra;
1 Samweli 13 : 17
17 ⑲ Nao watekaji wa nyara wakatoka katika kambi ya hao Wafilisti, vikosi vitatu; kikosi kimoja kikageukia njia iendayo Ofra, mpaka nchi ya Shuali;
2 Mambo ya Nyakati 13 : 19
19 ⑱ Abiya akamfuata Yeroboamu, akamnyang’anya miji, Betheli na vijiji vyake na Yeshana na vijiji vyake, na Efroni na vijiji vyake.
Yohana 11 : 54
54 Kwa hiyo Yesu hakutembea tena kwa wazi katikati ya Wayahudi; bali alitoka huko, akaenda mahali karibu na jangwa, mpaka mji uitwao Efraimu; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.
Waamuzi 6 : 11
11 Malaika wa BWANA akaenda akaketi chini ya mwaloni uliokuwa katika Ofra, uliokuwa mali yake Yoashi, Mwaabiezeri; na mwanawe Gideoni alikuwa akipepeta ngano ndani ya shinikizo, ili kuificha machoni pa Wamidiani.
Waamuzi 6 : 24
24 Ndipo Gideoni akamjengea BWANA madhabahu hapo, akaiita jina lake, Yehova-Shalomu;[8] hata hivi leo iko huko katika Ofra ya Waabiezeri.
Waamuzi 8 : 27
27 Basi Gideoni akafanya naivera kwa vitu vile, akaiweka katika mji wake, mji huo wa Ofra; nao Israeli wote wakaenda na kuiandama kwa ukahaba huko; nayo ilikuwa ni tanzi kwa Gideoni na kwa nyumba yake.
Waamuzi 8 : 32
32 Basi Gideoni mwana wa Yoashi akafa mwenye umri wa uzee mwema, akazikwa katika kaburi la Yoashi baba yake, katika Ofra ya Waabiezeri.
Waamuzi 9 : 5
5 Kisha akaenda nyumbani kwa babaye huko Ofra, akawaua nduguze, hao wana wa Yerubaali, watu sabini, akawaua juu ya jiwe moja; lakini Yothamu, mwana mdogo wa Yerubaali, alisalia; kwa maana alijificha.
1 Mambo ya Nyakati 4 : 14
14 Na Meonothai akamzaa Ofra; na Seraya akamzaa Yoabu, babaye Ge-harashimu;[3] kwani hao walikuwa mafundi stadi.
Leave a Reply