Biblia inasema nini kuhusu Onyx – Mistari yote ya Biblia kuhusu Onyx

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Onyx

Ayubu 28 : 16
16 Haiwezi kutiwa thamani kwa dhahabu ya Ofiri, Wala kwa shohamu ya thamani nyingi, wala kwa yakuti samawi.

Ezekieli 28 : 13
13 Ulikuwa ndani ya Adeni, bustani ya Mungu; kila jiwe la thamani lilikuwa kifuniko chako, akiki, na yakuti manjano, na almasi, na zabarajadi, na shohamu, na yaspi, na yakuti samawi, na zumaridi, na baharamani, na dhahabu; kazi ya matari yako na filimbi zako ilikuwa ndani yako; katika siku ya kuumbwa kwako zilitengenezwa tayari.

1 Mambo ya Nyakati 29 : 2
2 ⑱ Basi kwa uwezo wangu wote nimeiwekea akiba nyumba ya Mungu wangu, dhahabu kwa vitu vya dhahabu, na fedha kwa vitu vya fedha, na shaba kwa vitu vya shaba, na chuma kwa vitu vya chuma, na miti kwa vitu vya miti; vito vya shohamu, na vya kujazia, vito vya njumu, na vya rangi mbalimbali, na mawe ya thamani ya kila namna, na marumaru tele.

Ufunuo 21 : 20
20 wa tano sardoniki; wa sita akiki; wa saba krisolitho; wa nane zabarajadi; wa tisa yakuti ya manjano; wa kumi krisopraso; wa kumi na moja hiakintho; wa kumi na mbili amethisto.

Mwanzo 2 : 12
12 na dhahabu ya nchi ile ni njema; huko kuna bedola, na vito shoham.

Kutoka 28 : 12
12 Nawe utavitia vile vito viwili juu ya vipande vya mabegani vya hiyo naivera, viwe vito vya ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli; naye Haruni atayachukua majina yao mbele za BWANA juu ya mabega yake mawili ili kuwa ukumbusho.

Kutoka 28 : 20
20 na safu ya nne itakuwa ni zabarajadi, shohamu na yaspi; vito hivyo vitakazwa ndani ya dhahabu kwa kujaa mahali pake.

Kutoka 39 : 6
6 ⑧ Nao wakavitengeza vile vito vya shohamu, vilivyotiwa katika vijalizo vya dhahabu, vilivyochorwa mfano wa kuchora kwake mhuri, kwa majina ya hao wana wa Israeli.

Kutoka 39 : 13
13 ⑭ Na safu ya nne ilikuwa ni zabarajadi, na shohamu, na yaspi: vito hivyo vilikuwa vimetiwa katika vijalizo vya dhahabu, kila kimoja mahali pake.

Kutoka 25 : 7
7 na vito vya shohamu, na vito vingine vya kutiwa kwa ile naivera, na kwa kile kifuko cha kifuani.

Kutoka 35 : 9
9 na vito vya shohamu, vito vya kutiwa kwa hiyo naivera na kwa hicho kifuko cha kifuani.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *