Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Onan
Mwanzo 38 : 4
4 Akapata mimba tena, akazaa mwana, akamwita jina lake Onani.
Mwanzo 38 : 10
10 Jambo hili alilolifanya likawa baya machoni pa BWANA, basi akamwua yeye pia.
Mwanzo 46 : 12
12 Na wana wa Yuda; Eri, na Onani, na Shela, na Peresi, na Zera; lakini Eri na Onani walikufa katika nchi ya Kanaani. Na wana wa Peresi, ni Hesroni, na Hamuli.
Hesabu 26 : 19
19 Na wana wa Yuda, Eri na Onani; na hao Eri na Onani wakafa katika nchi ya Kanaani.
1 Mambo ya Nyakati 2 : 3
3 Wana wa Yuda; Eri, na Onani, na Shela; ambao hao watatu alizaliwa na binti Shua, Mkanaani. Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa BWANA; naye akamwua.
Leave a Reply