Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ofiri
Mwanzo 10 : 29
29 na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani.
1 Mambo ya Nyakati 1 : 23
23 na Ofiri, na Havila, na Yobabu. Hao wote ndio wana wa Yoktani.
1 Wafalme 9 : 28
28 Wakafika Ofiri, wakachukua toka huko dhahabu, talanta[20] mia nne na ishirini, wakamletea mfalme Sulemani.
1 Wafalme 10 : 11
11 Tena merikebu za Hiramu, zilizochukua dhahabu kutoka Ofiri, zikaleta kutoka Ofiri miti ya msandali mingi sana, na vito vya thamani.
2 Mambo ya Nyakati 8 : 18
18 ④ Naye Hiramu akamletea merikebu kwa mikono ya watumishi wake, na watumishi waliokuwa wanamaji; nao wakafika Ofiri pamoja na watumishi wa Sulemani, wakachukua kutoka huko talanta mia nne na hamsini za dhahabu, wakamletea mfalme Sulemani.
2 Mambo ya Nyakati 9 : 10
10 ⑦ Tena watumishi wa Hiramu, pamoja na watumishi wa Sulemani, walioleta dhahabu kutoka Ofiri, wakaleta miti ya msandali, na vito vya thamani.
1 Wafalme 22 : 48
48 Yehoshafati akafanya merikebu za Tarshishi ziende Ofiri kuchukua dhahabu; lakini hazikuenda; kwa maana merikebu zilivunjika huko Esion-geberi.
1 Mambo ya Nyakati 29 : 4
4 ⑳ yaani, talanta elfu tatu za dhahabu, za dhahabu ya Ofiri, na talanta elfu saba za fedha iliyosafika, ya kuzifunikiza kuta za nyumba;
Ayubu 22 : 24
24 Nawe hazina zako ziweke mchangani, Na dhahabu ya Ofiri iweke kati ya mawe ya vijito;
Ayubu 28 : 16
16 Haiwezi kutiwa thamani kwa dhahabu ya Ofiri, Wala kwa shohamu ya thamani nyingi, wala kwa yakuti samawi.
Zaburi 45 : 9
9 Binti za wafalme wamo Miongoni mwa akina bibi wako wastahiki. Katika mkono wako wa kulia amesimama malkia Akiwa amevaa dhahabu safi ya Ofiri.
Isaya 13 : 12
12 nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri.
Leave a Reply