Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Obadia
1 Wafalme 18 : 4
4 ⑱ kwa kuwa ikawa, Yezebeli alipowaua manabii wa BWANA, Obadia akatwaa manabii mia moja, akawaficha hamsini hamsini katika pango, akawalisha chakula na kuwapa maji).
1 Wafalme 18 : 16
16 Basi, Obadia akaenda zake amwone Ahabu, akamwambia; naye Ahabu akaenda kumlaki Eliya.
1 Mambo ya Nyakati 3 : 21
21 Na wana wa Hanania; Pelatia na Yeshaya; na wana wa Refaya, na wana wa Arnani, na wana wa Obadia, na wana wa Shekania.[1]
1 Mambo ya Nyakati 7 : 3
3 Na wana wa Uzi; Izrahia; na wana wa Izrahia; Mikaeli, na Obadia, na Yoeli, na Ishia, watano; wote wakuu.
1 Mambo ya Nyakati 8 : 38
38 naye Aseli alikuwa na wana sita, ambao majina yao ni haya; Azrikamu, na Bokeru, na Ishmaeli, na Shearia, na Obadia, na Hanani. Hao wote walikuwa wana wa Aseli.
1 Mambo ya Nyakati 9 : 44
44 naye Aseli alikuwa na wana sita, ambao majina yao ni haya; Azrikamu, na Bokeru, na Ishmaeli, na Shearia, na Obadia, na Hanani. Hao wote walikuwa wana wa Aseli.
1 Mambo ya Nyakati 9 : 16
16 na Obadia, mwana wa Shemaya, mwana wa Galali, mwana wa Yeduthuni; na Berekia, mwana wa Asa, mwana wa Elkana; waliokaa katika vijiji vya Wanetofathi.
1 Mambo ya Nyakati 12 : 9
9 Ezeri mkubwa wao, Obadia wa pili, Eliabu wa tatu;
1 Mambo ya Nyakati 27 : 19
19 wa Zabuloni, Ishmaya mwana wa Obadia; wa Naftali, Yeremothi mwana wa Azrieli;
2 Mambo ya Nyakati 17 : 9
9 ⑩ Wakafundisha katika Yuda, wenye kitabu cha Torati ya BWANA; wakazunguka katika miji yote ya Yuda, wakafundisha kati ya watu.
2 Mambo ya Nyakati 34 : 12
12 ⑩ Nao watu wakatenda kazi kwa uaminifu; na wasimamizi wao walikuwa Yahathi na Obadia, Walawi, wa wana wa Merari; na Zekaria na Meshulamu, wa wana wa Wakohathi, ili kuihimiza kazi; na wengine katika Walawi, wote waliokuwa mastadi wa kupiga vinanda.
Leave a Reply