Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Nzige
Mambo ya Walawi 11 : 22
22 ⑧ katika hao mna ruhusa kuwala; nzige kwa aina zake, na nzige kuu kwa aina zake, na panzi kwa aina zake, na parare kwa aina zake.
Mathayo 3 : 4
4 ⑥ Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
Marko 1 : 6
6 Na Yohana alikuwa amevaa singa za ngamia na mshipi wa ngozi kiunoni mwake, akala nzige na asali ya mwituni.
Kutoka 10 : 19
19 BWANA akaugeuza upepo wa magharibi wenye nguvu nyingi, ambao uliwaondoa wale nzige na kuwapeleka katika Bahari ya Shamu; hakusalia hata nzige mmoja ndani ya mipaka yote ya Misri.
Zaburi 105 : 35
35 Wakaila miche yote ya nchi yao, Wakayala matunda ya ardhi yao.
Kumbukumbu la Torati 28 : 38
38 Mbegu nyingi utazichukua nje shambani, lakini utavuna haba, kwa kuwa nzige watazila.
1 Wafalme 8 : 37
37 Ikiwa kuna njaa katika nchi, au tauni, au ukosefu wa mvua, au ukungu, au nzige, au panzi; ikiwa adui wamewazingira katika mji wao wowote ule;[17] au ukiwapo msiba wowote, au ugonjwa wowote;
2 Mambo ya Nyakati 7 : 13
13 Nikizifunga mbingu isiwepo mvua, tena nikiamuru nzige kula nchi, au nikiwatumia watu wangu tauni;
Isaya 33 : 4
4 Na mateka yako yatakukusanywa kama wadudu wakumbavyo, wataruka juu yake kama arukavyo nzige.
Yoeli 1 : 7
7 Ameuharibu mzabibu wangu; ameuvunja mtini wangu; ameyaambua magamba yake kabisa; ameuangusha chini; matawi yake yamefanywa kuwa meupe.
Ufunuo 9 : 10
10 Nao wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi mitano ilikuwa katika mikia yao.
Yoeli 2 : 2
2 siku ya giza na huzuni, siku ya mawingu na giza kuu. Kama mapambazuko yakitandazwa juu ya milima, hao ni wakuu, tena wenye nguvu, mfano wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi vingi.
Yoeli 2 : 10
10 Nchi inatetemeka mbele yao; mbingu zinatetemeka; jua na mwezi hutiwa giza, na nyota huacha kuangaza;
Mithali 30 : 27
27 Nzige hawana mfalme; Lakini huenda wote pamoja vikosi vikosi.
Waamuzi 6 : 5
5 Kwa maana walikwea na ng’ombe zao na hema zao, wakaja mfano wa nzige kwa wingi; wao na ngamia zao pia walikuwa hawana hesabu; nao waliingia katika hiyo nchi ili kuiharibu.
Waamuzi 7 : 12
12 ⑧ Nao Wamidiani na Waamaleki na, hao wana wa mashariki walikuwa wametua bondeni, mfano wa nzige kwa wingi; na ngamia wao walikuwa hawana hesabu; mfano wa mchanga wa ufuoni, kwa wingi.
Ayubu 39 : 20
20 Ndiwe uliyemfanya aruke kama nzige? Fahari ya mlio wake hutisha.
Yeremia 46 : 23
23 Wataukata msitu wake, asema BWANA, ingawa haupenyeki; Kwa maana ni wengi kuliko nzige, hawahesabiki.
Ufunuo 9 : 10
10 Nao wana mikia kama ya nge, na miiba; na nguvu yao ya kuwadhuru wanadamu miezi mitano ilikuwa katika mikia yao.
Leave a Reply