Biblia inasema nini kuhusu Nyumba ya Mungu – Mistari yote ya Biblia kuhusu Nyumba ya Mungu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Nyumba ya Mungu

Mathayo 21 : 13
13 ⑬ akawaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala; bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.

Marko 11 : 17
17 Akafundisha, akasema, Je! Haikuandikwa, Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.

Luka 19 : 46
46 akiwaambia, Imeandikwa, Nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala; lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.

Mhubiri 5 : 1
1 Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu; Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu; Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya.

Isaya 62 : 9
9 ② Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi BWANA; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu.

Ezekieli 43 : 12
12 ⑤ Hii ndiyo sheria ya nyumba; juu ya kilele cha mlima, mpaka wake wote pande zote patakuwa patakatifu sana. Tazama, hii ndiyo sheria ya nyumba.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *