Biblia inasema nini kuhusu Nyimbo za Nyimbo – Mistari yote ya Biblia kuhusu Nyimbo za Nyimbo

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Nyimbo za Nyimbo

2 Samweli 6 : 5
5 Daudi na nyumba yote ya Israeli wakacheza mbele za BWANA kwa nguvu zao zote, kwa nyimbo, na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa kayamba, na kwa matoazi.

1 Mambo ya Nyakati 13 : 8
8 Wakacheza Daudi na Israeli wote, mbele za Mungu, kwa nguvu zao zote; na kwa nyimbo na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa matoazi, na kwa tarumbeta.

1 Mambo ya Nyakati 16 : 5
5 Asafu mkuu wao, na wa pili wake Zekaria, na Yeieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Metithia, na Eliabu, na Benaya, na Obed-edomu, na Yeieli, wenye vinanda na vinubi; naye Asafu mwenye kupiga matoazi;

1 Mambo ya Nyakati 25 : 1
1 ⑤ Tena Daudi na makamanda wa jeshi wakatenga kwa utumishi baadhi ya wana wa Asafu, na wa Hemani, na wa Yeduthuni, watakaotabiri kwa vinubi na vinanda, na matoazi; hii ndiyo hesabu ya wafanya kazi kulingana na utumishi wao;

1 Mambo ya Nyakati 25 : 6
6 Hao wote waliamriwa na baba yao, waimbe nyumbani mwa BWANA, wakiwa na matoazi, vinanda, na vinubi, kwa utumishi wa nyumba ya Mungu; Asafu, Yeduthuni, na Hemani wakiwa wanaamriwa na mfalme.

2 Mambo ya Nyakati 29 : 25
25 ⑪ Akawasimamisha Walawi nyumbani mwa BWANA wenye matoazi, wenye vinanda, na wenye vinubi, kama alivyoamuru Daudi, na Gadi mwonaji wa mfalme, na Nathani nabii; kwani BWANA aliamuru hivi kwa manabii wake.

Zaburi 33 : 2
2 Mshukuruni BWANA kwa kinubi, Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa.

Zaburi 57 : 8
8 Amka, ee moyo wangu. Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri.

Zaburi 71 : 22
22 ⑭ Nami nitakushukuru kwa kinanda, Na kweli yako, Ee Mungu wangu. Nitakuimbia Wewe kwa kinubi, Ee Mtakatifu wa Israeli.

Zaburi 81 : 2
2 Pazeni zaburi, pigeni matari, Kinubi chenye sauti nzuri, na kinanda.

Zaburi 92 : 3
3 Kwa chombo chenye nyuzi kumi, Na kwa kinanda, Na kwa mlio wa kinubi.

Zaburi 108 : 2
2 Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri.

Zaburi 144 : 9
9 ⑥ Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya, Kwa kinanda chenye nyuzi kumi nitakuimbia.

Zaburi 150 : 3
3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu; Msifuni kwa kinanda na kinubi;

Ufunuo 5 : 8
8 Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana-kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato, ambayo ni maombi ya watakatifu.

Nehemia 12 : 27
27 ⑯ Basi, walipouweka wakfu ukuta wa Yerusalemu wakawatafuta Walawi katika mahali pao pote, ili kuwaleta Yerusalemu, ili waweze kusherehekea kuweka wakfu pamoja na furaha, na kwa shukrani, na kwa kuimba, kwa matoazi, vinanda na vinubi.

Danieli 3 : 5
5 wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zumari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha.

Danieli 3 : 7
7 Basi wakati huo, watu wa kabila zote walipoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zumari, na namna zote za ngoma, watu wote na mataifa na lugha wakaanguka, wakaiabudu ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha.

Danieli 3 : 10
10 Wewe, Ee mfalme, ulitoa amri ya kwamba kila mtu atakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zumari, na namna zote za ngoma, ni lazima aanguke na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *