Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Nyasi
Mwanzo 1 : 11
11 Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mimea itoayo mbegu, na miti ya matunda izaayo matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo.
Zaburi 72 : 6
6 ⑰ Atashuka kama mvua juu ya majani yaliyokatwa, Kama manyunyu yainyweshayo nchi.
Mathayo 6 : 30
30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa katika tanuri, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?
Luka 12 : 28
28 Basi, ikiwa Mungu huvika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo na kesho hutupwa katika tanuri, je! Hatawatendea ninyi zaidi, enyi wa imani haba?
Zaburi 129 : 6
6 ③ Na wawe kama majani ya darini Yanyaukayo kabla hayajamea.
Zaburi 90 : 6
6 ⑭ Asubuhi yachipuka na kumea, Jioni yakatika na kukauka.
Isaya 40 : 6
6 Sikiliza, ni sauti ya mtu asemaye, Lia! Nikasema, Nilie nini? Watu wote ni majani, Na wema wake wote ni kama ua la shambani;
1 Petro 1 : 24
24 Maana, Mwili wote ni kama majani, Na fahari yake yote ni kama ua la majani. Majani hukauka na ua lake huanguka;
Yakobo 1 : 11
11 Maana jua huchomoza kwa joto kali, huyakausha majani; ua lake huanguka, uzuri wa umbo lake hupotea; vivyo hivyo naye tajiri atanyauka katika njia zake.
Leave a Reply