Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Nondo
Ayubu 4 : 19
19 Je! Si zaidi sana hao wakaao katika nyumba za udongo, Ambazo misingi yao i katika mchanga, Hao wanaopondwa kama nondo!
Ayubu 27 : 18
18 Yeye hujenga nyumba yake kama mdudu, Na kama kibanda afanyacho mlinzi.
Zaburi 39 : 11
11 Ukimrudi mtu kwa kumkemea kwa uovu wake, Watowesha uzuri wake kama nondo. Kila mwanadamu ni ubatili.
Ayubu 13 : 28
28 Nijapokuwa ni kama kitu kilichooza, kinachosinyaa, Mfano wa nguo iliyoliwa na nondo.
Isaya 50 : 9
9 ⑤ Tazama, Bwana MUNGU atanisaidia; ni nani atakayenihukumu kuwa mwenye hatia? Tazama hao wote watachakaa kama vazi; nondo atawala.
Isaya 51 : 8
8 Maana nondo atawala kama vazi, na funza atawala kama sufu; bali haki yangu itakuwa ya milele, na wokovu wangu hata vizazi vyote.
Hosea 5 : 12
12 Kwa sababu hiyo mimi nimekuwa kama nondo kwa Efraimu, nimekuwa kama ubovu kwa nyumba ya Yuda.
Mathayo 6 : 20
20 bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wezi hawavunji wala hawaibi;
Yakobo 5 : 2
2 Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo.
Leave a Reply