Biblia inasema nini kuhusu njia – Mistari yote ya Biblia kuhusu njia

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia njia

Zaburi 119 : 105
105 Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu.

Mathayo 7 : 13
13 ⑱ Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.

Marko 1 : 1 – 45
1 Mwanzo wa Injili ya Yesu Kristo, Mwana wa Mungu.
2 Kama ilivyoandikwa katika nabii Isaya, Tazama, namtuma mjumbe wangu Mbele ya uso wako, Atakayeitengeneza njia yako.
3 Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.
4 Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi.
5 Wakamwendea nchi yote ya Yudea, nao wa Yerusalemu wote, wakabatizwa katika mto wa Yordani, wakiziungama dhambi zao.
6 Na Yohana alikuwa amevaa singa za ngamia na mshipi wa ngozi kiunoni mwake, akala nzige na asali ya mwituni.
7 Akahubiri akisema, Yuaja nyuma yangu aliye na nguvu kuliko mimi, ambaye mimi sistahili kuinama na kuilegeza gidamu ya viatu vyake.
8 Mimi niliwabatiza kwa maji; bali yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu.
9 Ikawa siku zile, Yesu alikuja kutoka Nazareti ya Galilaya, akabatizwa na Yohana katika Yordani.
10 Mara alipopanda kutoka majini, akaona mbingu zinapasuka, na Roho, kama hua, akishuka juu yake;
11 na sauti ikatoka mbinguni, Wewe ndiwe Mwanangu, mpendwa wangu; nimependezwa nawe.
12 Mara Roho akamtoa aende nyikani.
13 Akawako huko jangwani siku arubaini, hali akijaribiwa na Shetani; naye alikuwa pamoja na wanyama wa mwituni, na malaika walikuwa wakimhudumia.
14 Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu,
15 akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.
16 Naye alipokuwa akipita kando ya bahari ya Galilaya, akamwona Simoni na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi.
17 Yesu akawaambia, Njooni mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.
18 Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.
19 Akaendelea mbele kidogo, akamwona Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, nao pia walikuwa katika mashua, wakizitengeneza nyavu zao.
20 Mara akawaita, wakamwacha baba yao Zebedayo ndani ya mashua pamoja na wafanya kazi wakaenda, wakamfuata.
21 Wakashika njia mpaka Kapernaumu, na mara siku ya sabato akaingia katika sinagogi, akafundisha.
22 Wakashangaa mno kwa mafundisho yake; kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye mamlaka, wala si kama waandishi.
23 Na mara palikuwapo ndani ya sinagogi lao mtu mwenye pepo mchafu; akapaza sauti,
24 akisema, Tuna nini nawe, Yesu wa Nazareti? Je! Umekuja kutuangamiza?
25 Nakutambua u nani, Mtakatifu wa Mungu. Yesu akamkemea, akisema, Fumba kinywa, umtoke.
26 Yule pepo mchafu akamtia kifafa, akalia kwa sauti kuu, akamtoka.
27 Wakashangaa wote, hata wakaulizana, wakisema, Nini hii? Ni elimu mpya! Maana kwa uweza awaamuru hata pepo wachafu, nao wamtii!
28 Habari zake zikaenea haraka kote katika nchi zote kandokando ya Galilaya.
29 Na mara walipotoka katika sinagogi, walifika nyumbani kwa Simoni na Andrea, pamoja na Yakobo na Yohana.
30 Naye mkwewe Simoni, mamaye mkewe, alikuwa kitandani, akiugua homa; na mara wakamwambia habari zake.
31 Akamkaribia, akamwinua kwa kumshika mkono, homa ikamwacha, akaanza kuwatumikia.
32 Hata kulipokuwa jioni, na jua limekwisha kuchwa, walikuwa wakimletea wote waliokuwa wagonjwa, na wenye pepo.
33 Na mji wote ulikuwa umekusanyika mlangoni.
34 Akaponya wengi waliokuwa na maradhi mbalimbali, akatoa pepo wengi, wala hakuwaacha pepo kunena, kwa sababu walimjua.
35 Hata alfajiri na mapema sana akaondoka, akatoka akaenda zake mahali pasipokuwa na watu, akaomba huko.
36 Simoni na wenziwe wakamfuata;
37 nao walipomwona wakamwambia, Watu wote wanakutafuta.
38 Akawaambia, Twendeni mahali pengine, katika vijiji vilivyo karibu, nipate kuhubiri huko nako; maana nilikuja kwa ajili ya hilo.
39 Akaenda akihubiri katika masinagogi yao, katika nchi yote ya Galilaya, na kutoa pepo.
40 Akaja kwake mtu mwenye ukoma, akamsihi na kumpigia magoti, na kumwambia, Ukitaka, waweza kunitakasa.
41 Naye akamhurumia, akanyosha mkono wake, akamgusa, akamwambia, Nataka, takasika.
42 Na mara ukoma wake ukamtoka, akatakasika.
43 Akamkataza kwa nguvu, akamwondoa mara,
44 akamwambia, Angalia, usimwambie mtu neno lolote, ila nenda zako ukajioneshe kwa kuhani, ukatoe alivyoamuru Musa kwa ajili ya kutakasika kwako, iwe ushuhuda kwao.
45 Lakini akatoka, akaanza kuhubiri maneno mengi, na kulitangaza lile neno, hata Yesu asiweze tena kuingia mjini waziwazi; bali alikaa nje mahali pasipokuwa na watu, wakamwendea kutoka kila upande.

Yohana 14 : 6
6 ⑤ Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *