Biblia inasema nini kuhusu Nira, Kielelezo – Mistari yote ya Biblia kuhusu Nira, Kielelezo

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Nira, Kielelezo

Mambo ya Walawi 26 : 13
13 Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, niliyewaleta mtoke katika nchi ya Misri, ili msiwe watumwa wao; nami nimeivunja miti ya kongwa lenu, nikawafanya mwende sawasawa.

Isaya 9 : 4
4 ⑥ Kwa maana umeivunja nira ya mzigo wake, na gongo la bega lake, na fimbo yake yeye aliyemwonea, kama katika siku ya Midiani.

Isaya 10 : 27
27 Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta.

Yeremia 2 : 20
20 Kwa maana tangu zamani wewe umeivunja nira yako, na kuvipasua vifungo vyako; ukasema, Mimi sitatumika; kwa maana juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti wenye majani mabichi, umejiinamisha, ukafanya mambo ya ukahaba.

Yeremia 5 : 5
5 ⑮ nitawaendea watu wakubwa, nami nitasema nao; kwa maana hao wanaijua njia ya BWANA, na hukumu ya Mungu wao. Bali hawa kwa nia moja wameivunja nira, na kuvikata vifungo.

Yeremia 28 : 2
2 BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nimeivunja nira ya mfalme wa Babeli.

Yeremia 28 : 4
4 Nami nitamrudisha hapa Yekonia, mwana wa Yehoyakimu, mfalme wa Yuda, pamoja na mateka wote wa Yuda, waliokwenda Babeli, asema BWANA; maana nitaivunja nira ya mfalme wa Babeli.

Yeremia 28 : 10
10 Ndipo nabii Hanania akaitwaa hiyo nira iliyokuwa juu ya shingo ya Yeremia, akaivunja.

Yeremia 30 : 8
8 Na itakuwa katika siku ile, asema BWANA wa majeshi, nitaivunja nira yake itoke shingoni mwako, nami nitavipasua vifungo vyako; wala wageni hawatamtumikisha tena;

Maombolezo 1 : 14
14 Kongwa la makosa yangu limefungwa na mkono wake; Hayo yameshikamana; Yamepanda juu shingoni mwangu; Amezikomesha nguvu zangu;

Maombolezo 3 : 27
27 Ni vema mwanadamu aichukue nira Wakati wa ujana wake.

Mathayo 11 : 30
30 kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi.

Matendo 15 : 10
10 Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulibeba.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *