Biblia inasema nini kuhusu nia – Mistari yote ya Biblia kuhusu nia

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia nia

Mathayo 6 : 1 – 18
1 Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.
2 Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu.
3 Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kulia;
4 sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
5 Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao.
6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi.
8 Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.
9 Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje,
10 Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.
11 Utupe leo riziki yetu.
12 Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
13 Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]
14 Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi.
15 Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
16 Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.
17 Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;
18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Mithali 21 : 2
2 ⑮ Kila njia ya mtu ni sawa machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huipima mioyo.

Wagalatia 1 : 10
10 Maana, sasa je! Ni wanadamu ninaowashawishi, au Mungu? Au nataka kuwapendeza wanadamu? Kama ningekuwa hata sasa nawapendeza wanadamu, singekuwa mtumwa wa Kristo.

1 Wathesalonike 2 : 4
4 bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuwekewe amana Injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu anayetupima mioyo yetu.

Mathayo 6 : 1
1 Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.

Wafilipi 2 : 3
3 Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu na amhesabu mwenziwe kuwa bora kuliko nafsi yake.

1 Samweli 16 : 7
7 Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.

1 Yohana 3 : 12
12 ⑮ si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.

1 Wakorintho 4 : 5
5 Basi ninyi msihukumu neno kabla ya wakati wake, hata ajapo Bwana; ambaye atayamulika yaliyositirika katika giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo kila mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.

Mhubiri 12 : 13 – 14
13 Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
14 ⑥ Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri, likiwa jema au likiwa baya.

Yakobo 4 : 1 – 17
1 Vita vyatoka wapi, na mapigano yaliyoko kati yenu yatoka wapi? Si humu, katika tamaa zenu zifanyazo vita katika viungo vyenu?
2 Mwatamani, wala hamna kitu, mwaua na kuona wivu, wala hamwezi kupata. Mwafanya vita na kupigana, wala hamna kitu kwa kuwa hamwombi!
3 Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu.
4 Enyi wazinzi, hamjui ya kwamba kuwa rafiki wa dunia ni kuwa adui wa Mungu? Basi kila atakaye kuwa rafiki wa dunia hujifanya kuwa adui wa Mungu.
5 Au mwadhani ya kwamba Maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu?
6 Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu.
7 Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia.
8 Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili.
9 Huzunikeni na kuomboleza na kulia. Kucheka kwenu na kugeuzwe kuwa kuomboleza, na furaha yenu kuwa huzuni kubwa.
10 Jidhilini mbele za Bwana, naye atawakuza.
11 Ndugu, msisingiziane; amsingiziaye ndugu yake, au kumhukumu ndugu yake, huisingizia sheria na kuihukumu sheria. Lakini ukiihukumu sheria, huwi mtenda sheria, bali umekuwa hakimu.
12 Mtoa sheria na mwenye kuhukumu ni mmoja tu, ndiye awezaye kuokoa na kuangamiza. U nani wewe umhukumuye mtu mwingine?
13 Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida;
14 lakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa muda mfupi tu, kisha hutoweka.
15 Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi.
16 Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya.
17 Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.

1 Timotheo 1 : 5
5 Lakini lengo la agizo hili ni kuleta upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki.

1 Yohana 4 : 1
1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zipimeni hizo roho, kama zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.

Mwanzo 4 : 7
7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, lakini yapasa uishinde.

1 Wathesalonike 2 : 6 – 12
6 Hatukutafuta utukufu kwa wanadamu, wala kwenu, wala kwa wengine, ingawa tungeweza kuwalemea kama Mitume wa Kristo;
7 bali tulikuwa wapole katikati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe.
8 Hivyo ndivyo nasi tukiwajali kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapa, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.
9 Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu awaye yote, huku tukiwahubiria Injili ya Mungu.
10 Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa;
11 vile vile, kama mjuavyo, jinsi tulivyomwonya kila mmoja wenu kama baba awaonyavyo watoto wake mwenyewe, tukiwatia moyo na kushuhudia;
12 ili mwende kama ilivyo wajibu wenu kwa Mungu, mwenye kuwaita ninyi ili mwingie katika ufalme wake na utukufu wake.

Mithali 16 : 2
2 ⑧ Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huzipima roho za watu.

Mathayo 10 : 28
28 ⑤ Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika Jehanamu.

Hesabu 32 : 1 – 33
1 ③ Basi wana wa Reubeni, na hao wana wa Gadi, walikuwa na wanyama wa mifugo wengi sana; nao walipoona nchi ya Yazeri, na nchi ya Gileadi, ya kuwa mahali hapo palikuwa ni mahali pa kuwafaa wanyama;
2 hao wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, wakamwendea Musa na Eleazari kuhani, na wakuu wa mkutano, wakanena nao, wakisema,
3 Atarothi, na Diboni, na Yazeri, na Nimra, na Heshboni, na Eleale, na Sebamu, na Nebo na Beoni,
4 ④ nchi hiyo ambayo BWANA aliipiga mbele ya mkutano wa Israeli, ni nchi ifaayo kwa mifugo, nasi watumishi wako tunayo mifugo.
5 Wakasema, Kama tumepata kibali mbele ya macho yako, sisi watumishi wako na tupewe nchi hii iwe milki yetu; usituvushe mto wa Yordani.
6 Musa akawaambia wana wa Gadi na wana wa Reubeni, Je! Ndugu zenu waende vitani nanyi mtaketi hapa?
7 Mbona mwawavunja mioyo yao wana wa Israeli, wasivuke na kuingia nchi hiyo ambayo BWANA amewapa?
8 ⑤ Ndivyo walivyofanya baba zenu, hapo nilipowatuma kutoka Kadesh-barnea ili waende kuiangalia hiyo nchi.
9 ⑥ Kwa kuwa walipokwea na kuingia bonde la Eshkoli, na kuiona nchi, wakawavunja mioyo wana wa Israeli, ili wasikwee kuingia nchi aliyowapa BWANA.
10 ⑦ Na siku ile hasira za BWANA ziliwaka, naye akaapa, akisema,
11 ⑧ Hakika yangu hapana mtu mmoja katika wale watu waliotoka Misri, tangu huyo aliyepata umri wa miaka ishirini, na zaidi, atakayeiona hiyo nchi niliyomwapia Abrahamu, na Isaka, na Yakobo; kwa sababu hawakuniandama kwa moyo wote;
12 ⑩ ila Kalebu mwana wa Yefune, Mkenizi, na Yoshua mwana wa Nuni; kwa kuwa wao wamemwandama BWANA kwa moyo wote.
13 ⑪ Na hasira za BWANA ziliwaka juu ya Israeli, naye akawatembeza huku na huko jangwani muda wa miaka arubaini, hata kizazi hicho kizima kilichokuwa kimefanya uovu machoni pa BWANA kilipoisha angamia.
14 ⑫ Na tazama, ninyi kizazi cha watu wenye dhambi, mmeinuka badala ya baba zenu ili kuongeza tena hizo hasira kali za BWANA juu ya Israeli.
15 ⑬ Kwa kuwa mkigeuka msimfuate, yeye atawaacha tena nyikani; nanyi mtawaangamiza watu hawa wote.
16 Basi wakamwendea karibu, na kusema, Sisi tutafanya mazizi hapa kwa ajili ya mifugo yetu, na kujenga miji kwa ajili ya watoto wetu;
17 ⑭ lakini sisi wenyewe tutakuwa tayari na silaha zetu kutangulia mbele[44] ya wana wa Israeli, hata tutakapowafikisha mahali pao; na watoto wetu watakaa katika hiyo miji yenye maboma, kwa sababu ya wenyeji wa nchi.
18 ⑮ Sisi hatutarudia nyumba zetu, hata wana wa Israeli watakapokuwa wamekwisha kurithi kila mtu urithi wake.
19 ⑯ Kwa kuwa sisi hatutarithi pamoja nao huko ng’ambo ya pili ya Yordani, huko mbele; kwa sababu urithi wetu umetuangukia upande huu wa Yordani mwa mashariki.
20 ⑰ Basi Musa akawaambia, Kama mtafanya jambo hili; kama mtajivika silaha, ili kutangulia mbele ya BWANA mwende vitani,
21 tena kama kila mume wa kwenu mwenye kuchukua silaha atavuka Yordani mbele ya BWANA, hata atakapokuwa amekwisha watoa adui zake mbele yake,
22 ⑱ na hiyo nchi kushindwa mbele za BWANA; ndipo baadaye mtarudi, nanyi mtakuwa hamna hatia mbele za BWANA, wala kwa Israeli; na nchi hii itakuwa milki yenu mbele za BWANA.
23 ⑲ Lakini kama hamtaki kufanya neno hilo, ninyi mmefanya dhambi mbele za BWANA, nanyi jueni ya kwamba hiyo dhambi yenu itawapata, hapana budi.
24 ⑳ Basi, jengeni miji kwa ajili ya watoto wenu, na mazizi kwa ajili ya kondoo zenu; mkayafanye hayo mliotamka kwa vinywa vyenu.
25 Ndipo wana wa Gadi na wana wa Reubeni wakanena na Musa, na kumwambia, Sisi watumishi wako tutafanya kama wewe bwana wangu utuagizavyo.
26 Watoto wetu, na wake wetu, na kondoo wetu, na ng’ombe wetu wote, watakuwa hapo katika miji ya Gileadi;
27 lakini sisi watumishi wako tutavuka, kila mwanamume aliyevaa silaha za vita, mbele za BWANA, tuende vitani, kama wewe bwana wangu usemavyo.
28 Basi Musa akamwagiza Eleazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni, na wakuu wa nyumba za mababa za makabila ya wana wa Israeli, kuhusu watu hao.
29 Musa akawaambia, Kwamba wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, watavuka Yordani pamoja nanyi, kila mtu akiwa amevaa silaha kwa vita, mbele za BWANA, nayo nchi itashindwa mbele yenu; ndipo mtawapa nchi ya Gileadi kuwa milki yao;
30 lakini ikiwa hawataki kuvuka pamoja nanyi, wakiwa wamevaa silaha zao, ndipo watakuwa na milki zao kati yenu katika nchi ya Kanaani.
31 Wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, wakajibu na kusema, Kama BWANA alivyotuambia sisi watumishi wako, ndivyo tutakavyofanya.
32 Tutavuka, tukiwa tumevaa silaha zetu, mbele za BWANA, kuingia nchi ya Kanaani, nayo milki ya urithi wetu itakuwa ng’ambo ya pili[45] ya Yordani.
33 Basi Musa akawapa wao, maana, wana wa Gadi, na wana wa Reubeni, na hiyo nusu ya kabila la Manase, mwana wa Yusufu, ufalme wa Sihoni mfalme wa Waamori, na ufalme wa Ogu mfalme wa Bashani, hiyo nchi, kama miji yao ilivyokuwa, pamoja na mipaka yake, maana, miji ya hiyo nchi iliyozunguka kotekote.

1 Wathesalonike 2 : 1 – 12
1 Maana ninyi wenyewe, ndugu, mnakujua kuingia kwetu kwenu, ya kwamba hakukuwa bure;
2 ingawa tuliteswa na kutukanwa, katika Filipi kama mjuavyo, tulithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana.
3 Kwa maana maonyo yetu siyo ya ukosefu, wala ya uchafu, wala ya hila;
4 bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuwekewe amana Injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu anayetupima mioyo yetu.
5 Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wowote, kama mjuavyo, wala maneno ya juu juu ya kuficha choyo; Mungu ni shahidi.
6 Hatukutafuta utukufu kwa wanadamu, wala kwenu, wala kwa wengine, ingawa tungeweza kuwalemea kama Mitume wa Kristo;
7 bali tulikuwa wapole katikati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe.
8 Hivyo ndivyo nasi tukiwajali kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapa, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.
9 Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu awaye yote, huku tukiwahubiria Injili ya Mungu.
10 Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa;
11 vile vile, kama mjuavyo, jinsi tulivyomwonya kila mmoja wenu kama baba awaonyavyo watoto wake mwenyewe, tukiwatia moyo na kushuhudia;
12 ili mwende kama ilivyo wajibu wenu kwa Mungu, mwenye kuwaita ninyi ili mwingie katika ufalme wake na utukufu wake.

Mathayo 18 : 1 – 35
1 Saa ile wanafunzi wakamwendea Yesu wakisema,
2 Ni nani basi aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni? Akaita mtoto mmoja, akamweka katikati yao,
3 akasema, Amin, nawaambia, Msipoongoka na kuwa kama watoto, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
4 Basi, yeyote ajinyenyekezaye mwenyewe kama mtoto huyu, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme wa mbinguni.
5 Na yeyote atakayempokea mtoto mmoja mfano wa huyu kwa jina langu, anipokea mimi;
6 bali atakayemkosesha mmojawapo wa wadogo hawa waniaminio, yamfaa afungiwe shingoni jiwe kubwa la kusagia, na kutoswa katika kilindi cha bahari.
7 Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletaye jambo la kukosesha!
8 Basi mkono wako au mguu wako ukikukosesha, ukate ukautupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa umepungukiwa na mkono au mguu, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele.
9 Na jicho lako likikukosesha, ling’oe, ukalitupe mbali nawe; ni afadhali kuingia katika uzima ukiwa na chongo, kuliko kuwa na macho mawili, na kutupwa katika Jehanamu ya moto.
10 ① Angalieni msidharau mmojawapo wa wadogo hawa; kwa maana nawaambia ya kwamba malaika wao mbinguni siku zote huutazama uso wa Baba yangu aliye mbinguni. [
11 ② Kwa maana Mwana wa Adamu alikuja kukiokoa kilichopotea.]
12 ③ Mwaonaje? Mtu akiwa na kondoo mia, mmoja akampotea, je! Hawaachi wale tisini na tisa, akaenda milimani, na kumtafuta yule aliyepotea?
13 Hata akipata kumwona, amin, nawaambia, amfurahia huyo zaidi, kuliko wale tisini na tisa wasiopotea.
14 Vivyo hivyo haipendezi mbele za Baba yenu aliye mbinguni kwamba mmoja wa wadogo hawa apotee.
15 ④ Na ndugu yako akikukosea, nenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo.
16 ⑤ La, kama hasikii, chukua pamoja nawe tena mtu mmoja au wawili, ili kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno lithibitike.
17 ⑥ Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa; na asipolisikiliza kanisa pia, na awe kwako kama mtu wa mataifa na mtoza ushuru.
18 ⑦ Amin, nawaambieni, yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.
19 ⑧ Tena nawaambia, ya kwamba wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni.
20 ⑩ Kwa kuwa walipo wawili watatu wamekusanyika kwa jina langu, nami nipo papo hapo katikati yao.
21 ⑪ Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba?
22 Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.
23 Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumwa wake.
24 Alipoanza kuifanya, aliletewa mtu mmoja mwenye deni la talanta[5] elfu kumi.
25 Naye alipokosa cha kulipa, bwana wake akaamuru auzwe, yeye na mkewe na watoto wake, na vitu vyote alivyokuwa navyo, ikalipwe ile deni.
26 Basi yule mtumwa akaanguka, akamsujudia akisema, Bwana, nivumilie, nami nitakulipa yote pia.
27 Bwana wa mtumwa yule akamhurumia, akamfungua, akamsamehe ile deni.
28 Mtumwa yule akatoka, akamwona mmoja wa watumishi wake, aliyemwia dinari[6] mia; akamkamata, akamkaba koo, akisema, Nilipe unachodaiwa.
29 Basi mtumwa mwenzake akaanguka miguuni pake, akamsihi, akisema, Nivumilie, nami nitakulipa yote pia.
30 Lakini hakutaka, akaenda, akamtupa gerezani, hadi atakapoilipa ile deni.
31 Basi watumwa wenzake walipoyaona yaliyotendeka, walisikitika sana, wakaenda wakamweleza bwana wao yote yaliyotendeka.
32 Ndipo bwana wake akamwita, akamwambia, Ewe mtumwa mwovu, nilikusamehe wewe deni ile yote, uliponisihi;
33 nawe, je! Haikukupasa kumrehemu mtumwa mwenzako, kama mimi nilivyokurehemu wewe?
34 ⑫ Bwana wake akaghadhibika, akampeleka kwa watesaji, hata atakapoilipa deni ile yote.
35 ⑬ Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *