Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ngozi
2 Wafalme 1 : 8
8 Wakamwambia, Alikuwa amevaa vazi la manyoya, tena amejifunga shuka ya ngozi kiunoni mwake. Naye akasema, Ndiye yule Eliya Mtishbi.
Mathayo 3 : 4
4 ⑥ Naye Yohana mwenyewe alikuwa na vazi lake la singa za ngamia, na mshipi wa ngozi kiunoni mwake; na chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni.
Matendo 9 : 43
43 Basi Petro akakaa siku kadhaa huko Yafa, nyumbani mwa mtu mmoja, jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi.
Matendo 10 : 6
6 Yeye ni mgeni wa mtu mmoja, jina lake Simoni, mtengenezaji wa ngozi, ambaye nyumba yake iko pwani, atakuambia yakupasayo kutenda.
Mwanzo 3 : 21
21 BWANA Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.
Marko 1 : 6
6 Na Yohana alikuwa amevaa singa za ngamia na mshipi wa ngozi kiunoni mwake, akala nzige na asali ya mwituni.
Mambo ya Walawi 8 : 17
17 Lakini huyo ng’ombe mwenyewe, na ngozi yake, na nyama yake, na mavi yake, akaviteketeza nje ya kambi; vile vile kama BWANA alivyomwagiza Musa.
Leave a Reply