Biblia inasema nini kuhusu Ngome – Mistari yote ya Biblia kuhusu Ngome

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ngome

Mwanzo 25 : 16
16 ⑲ Hao ndio wana wa Ishmaeli, na hayo ni majina yao, katika miji yao, na katika vituo vyao, maseyidi kumi na wawili kwa kufuata jamaa zao.

Hesabu 31 : 10
10 Na miji yao yote, kila mahali walipokuwa wakikaa, na kambi yao yote wakayateketeza kwa moto.

1 Mambo ya Nyakati 11 : 5
5 Na hao wenyeji wa Yebusi wakamwambia Daudi, Hutaingia humu. Walakini Daudi akaitwaa ngome ya Sayuni; huu ndio mji wa Daudi.

1 Mambo ya Nyakati 11 : 7
7 ⑦ Basi Daudi akakaa ngomeni; kwa hiyo ukaitwa mji wa Daudi.

2 Mambo ya Nyakati 17 : 12
12 Ukuu wake Yehoshafati ukazidi sana; akajenga katika Yuda ngome na miji ya hazina.

2 Mambo ya Nyakati 27 : 4
4 Tena akajenga miji katika milima ya Yuda, na mwituni akajenga ngome na minara.

Matendo 21 : 34
34 Wengine katika makutano wakapiga kelele wakisema hivi, na wengine hivi. Basi alipokuwa hawezi kupata hakika ya habari kwa sababu ya zile kelele, akatoa amri aletwe ndani ya ngome.

Matendo 21 : 37
37 Naye alipokuwa analetwa ndani ya ngome, Paulo akamwambia jemadari, Nina ruhusa nikuambie neno? Naye akasema, Je! Unajua Kigiriki?

Matendo 23 : 10
10 Ugomvi mkubwa ulipotokea, yule jemadari akahofia Paulo asije akararuliwa nao, akaamuru askari washuke na kumwondoa kwa nguvu mikononi mwao, na kumleta ndani ya ngome.

Matendo 23 : 16
16 Mjomba wake Paulo akasikia habari za kuotea kwao, akaenda akaingia ndani ya ngome akampasha Paulo habari.

Matendo 23 : 32
32 hata asubuhi wakawaacha wale wapanda farasi waende pamoja naye, nao wakarudi zao ngomeni.

Mithali 18 : 19
19 Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuliko mji wa nguvu; Na mashindano ni kama mapingo ya ngome.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *