Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Neno la Mungu
Zaburi 40 : 7
7 ⑰ Ndipo niliposema, Tazama nimekuja, (Katika gombo la kitabu nimeandikiwa,)
Ufunuo 22 : 19
19 Na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mungu atamwondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima, na katika ule mji mtakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki.
Isaya 34 : 16
16 Tafuteni katika kitabu cha BWANA mkasome; hapana katika hao wote atakayekosa kuwapo, hapana mmoja atakayemkosa mwenzake; kwa maana kinywa changu kimeamuru, na roho yake imewakusanya.
Nehemia 8 : 3
3 Akasoma humo mbele ya uwanja uliokuwa ukikabili lango la maji, tangu mapambazuko hata adhuhuri, mbele ya hao wanaume na wanawake, na wale walioweza kufahamu; na masikio ya watu wote yakasikiliza kitabu cha Torati.
Wagalatia 3 : 10
10 ⑥ Kwa maana wale wote walio wa matendo ya sheria, wako chini ya laana; maana imeandikwa, Amelaaniwa kila mtu asiyedumu katika yote yaliyoandikwa katika kitabu cha Torati, ayafanye.
Waraka kwa Waebrania 6 : 5
5 na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za wakati ujao,
Warumi 1 : 2
2 ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa kinywa cha manabii wake katika Maandiko Matakatifu;
2 Timotheo 3 : 15
15 ⑳ na ya kuwa tangu utotoni umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu.
Zaburi 1 : 2
2 Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
Isaya 30 : 9
9 Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya BWANA;
Warumi 3 : 2
2 ⑲ Kwafaa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu.
1 Petro 4 : 11
11 ③ Mtu akisema, na aseme kama asemaye maneno halisi ya Mungu; mtu akihudumu, na ahudumu kwa nguvu anazojaliwa na Mungu; ili Mungu atukuzwe katika mambo yote kwa Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye hata milele na milele. Amina.
1 Wakorintho 15 : 3
3 ⑩ Kwa maana niliwatolea ninyi hapo mwanzo yale niliyoyapokea mimi mwenyewe, ya kuwa Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo Maandiko;
Danieli 10 : 21
21 ⑬ Lakini nitakuambia yaliyoandikwa katika maandiko ya kweli; wala hapana anisaidiaye juu ya hao ila huyo Mikaeli, mkuu wenu.
Waefeso 6 : 17
17 ⑭ Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
Yakobo 1 : 23
23 Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.
1 Petro 2 : 2
2 Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;
Luka 11 : 28
28 ⑳ Lakini yeye alisema, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika.
Waraka kwa Waebrania 4 : 12
12 ⑳ Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena ni jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Leave a Reply