Biblia inasema nini kuhusu Nebo – Mistari yote ya Biblia kuhusu Nebo

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Nebo

Hesabu 32 : 3
3 Atarothi, na Diboni, na Yazeri, na Nimra, na Heshboni, na Eleale, na Sebamu, na Nebo na Beoni,

Hesabu 32 : 38
38 na Nebo, na Baal-meoni, (majina yake yalikuwa yamegeuzwa) na Sibma; nao wakaiita miji waliyoijenga majina mengine.

1 Mambo ya Nyakati 5 : 8
8 ① na Bela, mwana wa Azazi, mwana wa Shemaya, mwana wa Yoeli, aliyekaa huko Aroeri, hadi Nebo na Baal-meoni;

Isaya 15 : 2
2 Wanapanda juu hata Bayithi na Diboni, mpaka mahali palipo juu ili walie; juu ya Nebo na juu ya Medeba Wamoabi wanalia; Wana upaa juu ya vichwa vyao vyote; kila ndevu zimenyolewa.

Yeremia 48 : 1
1 Kuhusu Moabu. BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Ole wake Nebo! Kwa maana umeharibika; Kiriathaimu umeaibishwa, umetwaliwa; Misgabu umeaibishwa, nao umebomolewa.

Yeremia 48 : 22
22 na juu ya Diboni, na juu ya Nebo, na juu ya Beth-diblathaimu;

Kumbukumbu la Torati 32 : 50
50 ukafe katika kilima, huko ukweako, ukusanywe uwe pamoja na jamaa zako; kama alivyokufa nduguyo Haruni katika mlima wa Hori, akakusanywa awe pamoja na watu wake;

Kumbukumbu la Torati 34 : 1
1 Musa akapanda kutoka uwanda wa Moabu mpaka mlima Nebo, hata kilele cha Pisga kukabili Yeriko. BWANA akamwonesha nchi yote ya Gileadi hata Dani;

Ezra 2 : 29
29 Watu wa Nebo, hamsini na wawili.

Nehemia 7 : 33
33 Watu wa Nebo, hamsini na wawili.

Ezra 10 : 43
43 ⑳ Na wa wazawa wa Nebo; Yeieli, na Matithia, na Zabadi, na Zebina, na Ido, na Yoeli, na Benaya.

Isaya 46 : 1
1 Beli anaanguka chini, Nebo anainama; sanamu zao ziko juu ya wanyama, na juu ya ng’ombe; vitu vile mlivyokuwa mkivichukua huku na huku vimekuwa mzigo, mzigo wa kumlemea mnyama aliyechoka.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *