Biblia inasema nini kuhusu Ndoto – Mistari yote ya Biblia kuhusu Ndoto

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ndoto

Ayubu 20 : 8
8 Ataruka mfano wa ndoto, asionekane; Naam, atafukuzwa kama maono ya usiku,

Mhubiri 5 : 3
3 Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno.

Mhubiri 5 : 7
7 Maana ndivyo ilivyo katika habari za wingi wa ndoto, na ubatili, na maneno mengi; walakini wewe umche Mungu.

Mwanzo 20 : 3
3 Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mke wa mtu.

Mwanzo 28 : 12
12 ⑧ Akaota ndoto; na tazama, ngazi imesimamishwa juu ya nchi, na ncha yake yafika mbinguni. Tena, tazama, malaika wa Mungu wanapanda, na kushuka juu yake.

Mwanzo 31 : 13
13 Mimi ni Mungu wa Betheli, huko ulikotia mafuta nguzo, na kuniwekea nadhiri. Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa.

Mwanzo 46 : 2
2 Mungu akanena na Israeli katika ndoto ya usiku, akasema, Yakobo, Yakobo. Akasema, Mimi hapa.

Mwanzo 31 : 24
24 Mungu akamjia Labani, Mshami, katika ndoto ya usiku, akamwambia, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari.

Mwanzo 37 : 10
10 Akawaambia baba yake na ndugu zake; baba yake akamkemea akamwambia, Ni ndoto gani hii uliyoiota? Je! Mimi na mama yako na ndugu zako tutakuja tukusujudie mpaka chini?

Waamuzi 7 : 13
13 ⑩ Hata Gideoni alipofika, tazama, palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa akimhadithia mwenziwe ndoto, akasema, Tazama, niliota ndoto, na tazama, mkate wa shayiri ulianguka katika kambi ya Wamidiani, ukafika katika hema moja, ukaipiga hadi ikaanguka, ukaipindua, hadi ikalala chini.

1 Wafalme 3 : 15
15 ⑤ Naye Sulemani akaamka, na kumbe! Ni ndoto. Akaenda Yerusalemu, akasimama mbele ya sanduku la Agano la BWANA, akatoa sadaka za kuteketezwa, akatoa na sadaka za amani; akawafanyia karamu watumishi wake wote.

Ayubu 4 : 21
21 Je! Kamba ya hema yao haikung’olewa ndani yao? Nao hufa hata bila kuwa na hekima.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *