Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia ndoa ya jinsia moja
Mambo ya Walawi 18 : 22
22 ⑤ Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.
1 Wakorintho 6 : 9 – 10
9 Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti,
10 ⑪ wala wezi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang’anyi.
1 Timotheo 1 : 9 – 10
9 akilifahamu neno hili, ya kuwa sheria haimhusu mtu asiye na hatia, bali wavunjao sheria, waasi, na makafiri, na wenye dhambi, na wanajisi, na wasiomcha Mungu, na wapigao baba zao, na wapigao mama zao, na wauaji,
10 na wazinifu, na wafiraji, na waibao watu, na waongo, nao waapao kwa uongo; na linginelo lolote lisilopatana na mafundisho ya kweli;
Mathayo 19 : 4 – 6
4 ⑰ Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mwanamume na mwanamke,
5 ⑱ akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
6 ⑲ Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
Kumbukumbu la Torati 22 : 5
5 ⑰ Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.
Warumi 13 : 8 – 10
8 ③ Msiwiwe na mtu chochote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.
9 ④ Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yoyote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
10 ⑤ Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.
Marko 10 : 6 – 9
6 ⑥ Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwaumba mwanamume na mwanamke.
7 ⑦ Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;
8 na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
9 Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.
Mambo ya Walawi 20 : 13
13 ① Tena mwanamume akilala pamoja na mwanamume, kama alalavyo na mwanamke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.
Wagalatia 5 : 14
14 ⑩ Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako.
Wagalatia 3 : 28
28 Hakuna Myahudi wala Mgiriki. Hakuna mtumwa wala huru. Hakuna mwanamume wala mwanamke. Maana ninyi nyote mmekuwa wamoja katika Kristo Yesu.
Isaya 56 : 3 – 5
3 Wala mgeni, aambatanaye na BWANA, asiseme hivi, Hakika yake BWANA atanitenga na watu wake; wala towashi asiseme, Mimi ni mti mkavu.
4 Kwa maana BWANA awaambia hivi matowashi, wanaozishika sabato zangu, na kuyachagua mambo yanipendezayo, na kulishika sana agano langu;
5 Nitawapa hawa nyumbani mwangu, na ndani ya kuta zangu, kumbukumbu na jina, lililo jema kuliko kuwa na watoto wa kiume na wa kike; nitawapa jina lidumulo milele, lisilokatiliwa mbali.
Mathayo 19 : 11 – 12
11 Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.
12 Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.
2 Samweli 1 : 26
26 Nimesikitika kwa ajili yako, Yonathani, ndugu yangu, Ulikuwa ukinipendeza sana; Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu, Kupita upendo wa wanawake.
Mathayo 22 : 39
39 ① Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
1 Wakorintho 7 : 7 – 9
7 Ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo; lakini kila mtu ana karama yake mwenyewe itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi.
8 Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo.
9 Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.
1 Samweli 18 : 1 – 4
1 Ikawa Daudi alipokwisha kusema na Sauli, roho ya Yonathani, ikaambatana na roho ya Daudi, Yonathani akampenda kama roho yake mwenyewe.
2 Sauli akamtwaa siku ile, wala hakumwacha arudi tena nyumbani kwa baba yake.
3 Nao Yonathani na Daudi wakaahidiana, kwa kuwa alimpenda kama roho yake mwenyewe.
4 Ndipo Yonathani akalivua joho alilokuwa amelivaa, akampa Daudi, na mavazi yake, hata na upanga wake pia, na upinde wake, na mshipi wake.
Mathayo 7 : 12
12 ⑰ Basi yoyote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo Torati na Manabii.
Leave a Reply