Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ndoa
Mwanzo 11 : 29
29 Abramu na Nahori wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la mkewe Nahori aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa Iska.
Mwanzo 12 : 13
13 Tafadhali useme, wewe u ndugu yangu, iwe heri kwangu kwa ajili yako, na nafsi yangu iishi kwa ajili yako.
Mwanzo 20 : 3
3 Lakini Mungu akamjia Abimeleki katika ndoto ya usiku, akamwambia, Umekuwa mfu wewe kwa sababu ya mwanamke huyu uliyemtwaa, maana ni mke wa mtu.
Mwanzo 20 : 16
16 Naye akamwambia Sara, Tazama! Nimempa ndugu yako fedha elfu moja, itakuwa kifunika macho kwako mbele ya wote walio pamoja nawe, nawe utakuwa na haki mbele ya watu wote.
Mwanzo 24 : 4
4 ⑫ bali nenda hata nchi yangu, na kwa jamaa zangu, ukamtwalie mwanangu Isaka mke.
Mwanzo 24 : 67
67 Isaka akamwingiza Rebeka katika hema ya mama yake, Sara, akamtwaa Rebeka, akawa mkewe, akampenda; Isaka akafarijika kwa ajili ya kufa kwa mama yake.
Mwanzo 28 : 2
2 Ondoka, uende Padan-aramu, mpaka nyumba ya Bethueli baba ya mama yako, ukajitwalie huko mke katika binti za Labani, ndugu wa mama yako.
Mwanzo 29 : 30
30 Ndipo Yakobo[14] akaingia kwa Raheli, akampenda Raheli kuliko Lea, akatumika kwa ajili yake miaka saba mingine.
Mwanzo 38 : 8
8 Yuda akamwambia Onani, Uingie kwa mke wa nduguyo, ukamwoe, ukamwinulie nduguyo uzao.
Mwanzo 38 : 11
11 Yuda akamwambia Tamari mkwewe, Ukae mjane nyumbani mwa baba yako hata Shela mwanangu atakapokuwa mtu mzima, maana alisema, Asipate kufa yeye kama nduguze. Basi Tamari akaenda, akakaa nyumbani mwa babaye.
Kumbukumbu la Torati 25 : 10
10 Na jina lake katika Israeli liitwe, Nyumba ya mvuliwa kiatu.
Ruthu 4 : 5
5 ⑬ Ndipo Boazi aliposema, Siku ile utakapolinunua shamba mkononi mwa Naomi, unamnunua Ruthu pia, huyu Mmoabi, mkewe marehemu, ili makusudi umwinulie marehemu jina katika urithi wake.
Mathayo 22 : 24
24 wakisema, Mwalimu, Musa alisema, Mtu akifa, akiwa hana watoto, ndugu yake na amwoe yule mkewe, ili ampatie nduguye mzao.
Marko 12 : 23
23 Basi, katika kiyama atakuwa mke wa yupi katika hao? Maana wote saba walikuwa naye.
Luka 20 : 28
28 ⑬ wakisema, Mwalimu, Musa alituandikia ya kuwa, mtu akifiwa na ndugu yake mwenye mke, lakini hana mtoto na amtwae huyu mke, ampatie ndugu yake mzao.
Mwanzo 21 : 21
21 ⑰ Akakaa katika jangwa la Parani; mama yake akamtwalia mke katika nchi ya Misri.
Leave a Reply