Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia ndevu
Mambo ya Walawi 19 : 27
27 Msinyoe denge pembe za vichwani, wala msiharibu pembe za ndevu zenu.
Ezekieli 44 : 20
20 Hawatanyoa vichwa vyao, wala hawataacha nywele zao kuwa ndefu sana; watazipunguza nywele za vichwa vyao tu.
Mambo ya Walawi 21 : 5
5 ⑯ Wasijifanyie upara kichwani, wala wasinyoe pembe za ndevu zao, wala wasichanje tojo katika miili yao.
Isaya 50 : 6
6 ② Niliwatolea wapigao mgongo wangu, na wang’oao ndevu mashavu yangu; sikuficha uso wangu usipate fedheha na kutemewa mate.
Mithali 20 : 29
29 Fahari ya vijana ni nguvu zao, Na uzuri wa wazee ni kichwa chenye mvi.
Ezekieli 5 : 1
1 Nawe, mwanadamu, ujipatie upanga mkali, kama wembe wa kinyozi ujipatie, ukaupitishe juu ya kichwa chako na ndevu zako; kisha ujipatie mizani ya kupimia, ukazigawanye nywele hizo.
Yeremia 9 : 26
26 ⑲ Misri, na Yuda, na Edomu, na wana wa Amoni, na Moabu, na wote wenye kunyoa denge, wakaao nyikani; maana mataifa hayo yote hawana tohara, wala nyumba yote ya Israeli hawakutahiriwa mioyo yao.
Leave a Reply