Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ndege
Mwanzo 1 : 30
30 na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.
Mwanzo 1 : 26
26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila kiumbe kitambaacho nchini.
Mwanzo 1 : 28
28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuimiliki; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Mwanzo 9 : 3
3 Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapa hivi vyote.
Zaburi 8 : 8
8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini; Na kila kipitacho njia za baharini.
Yeremia 27 : 6
6 Na sasa nimetia nchi hizi zote katika mkono wa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu; na wanyama pori pia nimempa wamtumikie.
Danieli 2 : 38
38 na kila mahali wakaapo wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani amewatia mkononi mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote; wewe u kichwa kile cha dhahabu.
Yakobo 3 : 7
7 Maana kila aina ya wanyama, na ya ndege, na ya vitambaavyo, na ya vitu vilivyomo baharini, vinafugika, navyo vimekwisha kufugwa na wanadamu.
Mwanzo 9 : 3
3 Kila kiendacho kilicho hai kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapa hivi vyote.
Kumbukumbu la Torati 14 : 20
20 Mna ruhusa kula katika ndege wote walio safi.
Mambo ya Walawi 11 : 20
20 Tena vyote vitambaavyo vyenye mabawa viendavyo kwa miguu minne, hivi ni machukizo kwenu.
Ayubu 38 : 41
41 ⑪ Ni nani anayempatia kunguru chakula, Makinda yake wanapomlilia Mungu, Na kutangatanga kwa kutindikiwa na chakula?
Zaburi 147 : 9
9 Humpa mnyama chakula chake, Wana-kunguru waliao.
Mathayo 10 : 29
29 Je! Mashomoro wawili hawauzwi kwa senti moja? Wala hata mmoja haanguki chini asipojua Baba yenu;
Luka 12 : 6
6 Je! Shomoro watano hawauzwi kwa senti mbili? Wala hasahauliwi hata mmojawapo mbele za Mungu.
Luka 12 : 24
24 ① Watafakarini kunguru, ya kwamba hawapandi wala hawavuni; hawana ghala wala uchaga, lakini Mungu huwalisha. Bora ninyi mara nyingi kuliko ndege!
Zaburi 104 : 12
12 Kandokando hukaa ndege wa angani; Na kuimba wakiwa katika matawi.
Mhubiri 12 : 4
4 ③ Na milango kufungwa katika njia kuu; Sauti ya kinu itakapokuwa ni ndogo; Na mtu kushtuka kwa sauti ya ndege; Nao binti za kuimba watapunguzwa;
Wimbo ulio Bora 2 : 12
12 Maua yatokea katika nchi, Wakati wa kuimba umefika, Na sauti ya mwigo husikiwa kwetu.
Leave a Reply