Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Naftali
Mwanzo 30 : 8
8 Raheli akasema, Kwa mashindano makuu nimeshindana na dada yangu, nikashinda. Akamwita jina lake Naftali.
Mwanzo 35 : 25
25 Wana wa Bilha, kijakazi wa Raheli, ni Dani na Naftali.
Mwanzo 49 : 21
21 Naftali ni ayala aliyefunguliwa; Anatoa maneno mazuri.
Mwanzo 46 : 24
24 Na wana wa Naftali; Yaseeli, na Guni, na Yaseri, na Shilemu.
1 Mambo ya Nyakati 7 : 13
13 Wana wa Naftali; Yaseeli, na Guni, na Yeseri, na Shalumu; wana wa Bilha.
Hesabu 1 : 43
43 wale waliohesabiwa katika kabila la Naftali, walikuwa watu elfu hamsini na tatu na mia nne (53,400).
Hesabu 26 : 50
50 Hawa ndio jamaa wa Naftali kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa elfu arubaini na tano na mia nne.
Hesabu 2 : 31
31 ⑫ Wote waliohesabiwa katika kambi ya Dani walikuwa elfu mia moja hamsini na saba na mia sita. Hao ndio watakaoondoka mwisho kwa kufuata bendera[2] yao.
Hesabu 10 : 27
27 Tena juu ya jeshi la kabila la wana wa Naftali ni Ahira mwana wa Enani.
Kumbukumbu la Torati 33 : 23
23 Na Naftali akamnena, Ee Naftali, uliyeshiba fadhili, Uliyejawa na baraka ya BWANA; Umiliki magharibi na kusini.
Yoshua 19 : 39
39 Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Naftali kwa kufuata jamaa zao; miji hiyo pamoja na vijiji vyake.
Waamuzi 1 : 33
33 Naftali naye hakuwatoa wenyeji wa Beth-shemeshi, wala hao waliokaa Bethanathi; lakini alikaa kati ya Wakanaani, hao wenyeji wa nchi; pamoja na haya, hao wenyeji wa Beth-shemeshi, na wenyeji wa Bethi-anathi, wakawatumikia kazi ya shokoa.
Ezekieli 48 : 3
3 Na mpakani mwa Asheri, toka upande wa mashariki hadi upande wa magharibi; Naftali, fungu moja.
Waamuzi 4 : 6
6 Siku moja Debora akatuma mtu akamwita Baraka wa Abinoamu kutoka Kedesh-Naftali, akamwambia, BWANA, Mungu wa Israeli anakuamuru hivi: “Nenda, ukawaogoze watu elfu kumi na wana wa Naftali, na wa wana wa Zabuloni, ili washike doria katika mlima Tabori”.
Waamuzi 4 : 10
10 Baraka akawakutanisha Naftali na Zabuloni waende Kedeshi wakakwea watu elfu kumi wakimfuata; Debora naye akaenda pamoja naye.
Waamuzi 5 : 18
18 ⑬ Zabuloni ndio watu waliohatarisha roho zao hadi kufa; Nao Naftali mahali palipoinuka kondeni.
Waamuzi 6 : 35
35 Kisha akatuma wajumbe waende kati ya Manase yote; wao nao walikutana pamoja ili kumfuata; kisha akatuma wajumbe waende kwa Asheri, na kwa Zabuloni, na kwa Naftali; nao wakakwea ili kumlaki.
Waamuzi 7 : 23
23 Wanaume wa Israeli walikuwa wamekusanyika kutoka Naftali, na kutoka Asheri, na kutoka Manase yote, wakawafuata Midiani.
Leave a Reply