Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Mzeituni
Mwanzo 8 : 11
11 njiwa akamjia jioni, na tazama, alikuwa na jani bichi la mzeituni kinywani mwake, ambalo amelichuma, basi Nuhu akajua ya kwamba maji yamepunguka juu ya nchi.
Kutoka 23 : 11
11 lakini mwaka wa saba utaiacha nchi ipumzike na kutulia; hao maskini miongoni mwa watu wako wapate kula; na hicho watakachosaza wao, wapate kula wanyama wa kondeni. Utafanya vivyo hivyo katika shamba lako la mizabibu, na katika shamba lako la mizeituni.
Kumbukumbu la Torati 6 : 11
11 na nyumba zimejaa vitu vyema vyote usizojaza wewe, na visima vilivyochimbwa usivyochimba wewe, mashamba ya mizabibu na mizeituni usiyoipanda wewe, nawe utakula na kushiba;
Kumbukumbu la Torati 8 : 8
8 nchi ya ngano na shayiri, na mizabibu, na mitini, na mikomamanga; nchi ya mizeituni yenye mafuta, na asali;
Kumbukumbu la Torati 28 : 40
40 Utakuwa na mizeituni katika mipaka yako yote usijipake mafuta yake; kwa kuwa mzeituni wako utapukutika.
Nehemia 8 : 15
15 na ya kwamba wahubiri na kutangaza katika miji yao yote, na katika Yerusalemu, kusema, Nendeni mlimani, mkalete matawi ya mzeituni, na matawi ya mzeituni mwitu, na matawi ya mihadasi, na matawi ya mitende, na matawi ya miti minene, ili kufanya vibanda, kama ilivyoandikwa.
Ayubu 15 : 33
33 Atayapukutisha mapooza yake kama mzabibu, Na kuyatupa maua yake kama mzeituni.
Kumbukumbu la Torati 24 : 20
20 Utakapochuma matunda ya mizeituni yako, usirudi kuchuma mara ya pili; yaliyobaki apewe mgeni, na yatima, na mjane.
Isaya 17 : 6
6 Lakini kilichosazwa na mvunaji kitakuwa ndani yake, kama vile wakati wa kupiga mizeituni, matunda mawili matatu yaliyo juu sana; matunda manne matano katika matawi, matawi ya mti wa matunda, asema BWANA, Mungu wa Israeli.
1 Wafalme 6 : 23
23 Akafanya ndani ya chumba cha ndani makerubi mawili ya mzeituni, kwenda juu mikono kumi.
1 Wafalme 6 : 33
33 Ndivyo alivyoyafanyia maingilio ya hekalu miimo ya mzeituni, yenye pande nne;
Waamuzi 9 : 8
8 Siku moja miti ilitoka ili kuutia mmoja mafuta uwe mfalme juu yao; ikauambia mti mzeituni, Tawala wewe juu yetu.
Zaburi 128 : 3
3 Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Katika nyumba yako. Wanao watakuwa kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako.
Warumi 11 : 21
21 Kwa maana ikiwa Mungu hakuyaachia matawi ya asili, wala hatakuachia wewe.
Warumi 11 : 24
24 Kwa maana ikiwa wewe ulikatwa ukatolewa katika mzeituni, ulio mzeituni mwitu kwa asili yake, kisha ukapandikizwa, kinyume cha asili, katika mzeituni ulio mwema, si zaidi sana wale walio wa asili kuweza kupandikizwa katika mzeituni wao wenyewe?
Leave a Reply